Friday , 26 April 2024
Home Kitengo Michezo Tanzania yafuzu kombe la Dunia mchezo wa soka kwa wenye ulemavu
Michezo

Tanzania yafuzu kombe la Dunia mchezo wa soka kwa wenye ulemavu

Spread the love

 

TIMU ya Tanzania ya soka kwa wenye ulemavu ‘Tembo Warriors’ imefuzu kucheza kombe la dunia Uturuki 2022. Anaripoti John Mapepele, MAELEZO…(endelea).

Ni baada ya kuichapa Cameroon 5-0 leo Jumatano, tarehe 1 Desemba 2021, katika michuano ya Soka ya Bara la Afrika kwa wenye ulemavu (CANAF 2021), katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Kipigo hicho ilichokitoa kwa Cameroon, imewafanya Tembo Worriors kutinga fainali ya michuanbo hiyo, inayofanyikia viwanja vya Benjamin Mkapa, Uhuru na JK Park

Mchezo huo uliopigwa asubuhi, umeshuhudiwa na Waziri wa Sanaa, Utamaduni na Michezo, Innocent Bashungwa, Katibu Mkuu wake, Dk. Hassan Abbas na Rais wa Mashindano hayo duniani, Mateus Wildack.

Timu ya Tanzania ambayo katika kipindi chote cha maandalizi imesimamiwa na Kamati Maalum ya Kitaifa chini ya Dk. Abbasi ilianza vizuri kutokana hamasa iliyotolewa na Rais wa wa Tanzania, Samia Suluhu Hasan.

Katika mechi zote za mashindano haya Tanzania imepoteza mechi moja tu ya Uganda mbayo ilifungwa goli 1-0, ambapo Tembo iliifunga Morocco 2-1 na Sierra Leone 1-0.

Mara baada ya mchezo huo, Waziri Bashungwa amewahakikishia kwamba Serikali itaendelea kuiisaidia timu hiyo ili iendelee kufanya vizuri kwenye maandalizi ya Kombe la Dunia.

Naye Dk. Abbasi amesema kwa kuwa safari ya kuelekea kombe la dunia imekamilika kazi iliyobaki ni kuhakikisha kuwa kombe linabaki Tanzania.

Ushindi huo, dhidi ya Cameroon pia umeufanya timu hiyo kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano hiyo ambayo inafanyika hapa nchini.

Magoli mawili ya Tanzania yamefungwa na Alfan Kyanga dakika ya 2 na 15 , Ramadhan Chomole dakika ya 18, na Frank Ngailo dakika ya 36 na 44.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

EPL, Ligue 1 na Coppa Italia kinawaka leo

Spread the love  LEO ligi kadhaa zitaendelea nchini barani ulaya ikiwemo ligi...

BiasharaMichezo

NBC yaunga mkono jitihada kutokomeza malaria

Spread the loveKuelekea Maadhimisho ya siku ya malaria Duniani yatakayofanyika kesho Aprili...

Michezo

Arsenal dhidi ya Chelsea ngoma nzito leo EPL

Spread the love  Leo kutakua na mchezo mkali sana pale kwenye ligi...

Habari MchanganyikoMichezo

NBC yanogesha Derby Kariakoo, Aziz Ki aibuka mchezaji bora Machi

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) ambayo ni mdhamini Mkuu...

error: Content is protected !!