May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Waziri wa zamani Zanzibar ajitosa kumrithi Maalim Seif ACT-Wazalendo, ataja ahadi 10

Spread the love

 

MJUMBE wa Kamati Kuu, ya Chama cha ACT-Wazalendo, Hamad Masoud Hamad, ametangaza nia ya kugombea uenyekiti wa chama hicho, iliyoachwa wazi na Hayati Maalim Seif Shariff Hamad. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Hamad ametangaza nia hiyo leo Jumatano, tarehe 1 Desemba 2021, akizungumza na wanahabari mkoani Dar es Salaam.

Akizungumza na wanahabari hao, Hamad amesema anaweza kuvaa viatu vya Maalim Seif katika kuiongoza ACT-Wazalendo, kwani alifanya naye kazi kwa zaidi ya miaka 20, tangu akiwa Chama cha Wananchi (CUF), hadi alipohamia katika chama hicho 2019.

Waziri huyo wa zamani wa miundombinu na mawasiliano Zanzibar, ametaja vipaumbele zaidi ya 10, alivyoahidi kuvitekeleza endapo atachaguliwa kuwa Mwenyekiti wa ACT Wazalendo, katika mkutano wa dharura wa chama hicho unatarajiwa kufanyika tarege 19 Januari 2022.

Hamad ametaja vipaumbele hivyo ni, upatikanaji wa mamlaka kamili Zanzibar, kuimarisha na kudumisha maridhiano na Serikali ya Umoja wa Kitaifa (SUK), yaliyoanzishwa na marehemu Maalim Seif enzi za uhai wake.

“Nitaimarisha na kudumisha maridhiano yaliyoanzishwa na marehemu Maalim  Seif na aliyekuwa Rais wa Zanzibar, Aman Karume. Nitatoa msukumo mkubwa zaidi wa agenda mama ya Wazanzibar ya Zanzibar kuwa na mamlaka kamili pamoja na kulinda tunu ya kuwepo wa kudumisha SUK,” ameahidi Hamad.

Vipaumbele vingine ni, kuhakikisha ACT-Wazalendo kwa kushirikiana na vyama vingine vya siasa, kuleta msukumo wa  upatikanaji  Katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.

“Kwa kushirikiana na vyama vingime, taasisi mbalimbali na wadau wemgine kuleta maukumo na kuhakikisha upatikanaji wa katiba mpya na tume huru ya uchaguzi,” amesema Hamad.

Vilevile, Hamad amesema akifanikiwa kuwa Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo, atahakikisha sheria kandamizi zinarekebishwa.

“Katika uongozi wangu  nitaziibua, kuzipinga,  na kuzisemea  kwa nguvu zote sheria mbaya na kandamizi, uvunjwaji hovyo wa haki za binadamu, utawala bora. Pia nitaunganisha nguvu ya umma katika kuisimamia Serikali ifanye mabadiliko makubwa,” amesema Hamad.

Hamad amesema kuwa, kipaumbele chake kingine kitakuwa ni kukiimarisha  chama hicho katikangazi za majimbo, mikoa na Taifa, ikiwemo kubuni njia za kupata mapato kwa ajili ya kujiendesha.

“Chama kitajizatiti kuhakikisha hakiporwi ushindi wake katika chaguzi za Serikali za Mitaa na chaguzi kuu zijazo,” amesema Hamad.

Vipaumbele vingine vilivyotajwa na mwanasiasa huyo ni, kutanua mtandao wa ACT-wazalendo hususan Tanzania Bara ili ufanane na wa Zanzibar.

“Katika uongozi wangu nitahakikisha chama kinayaibua, kuyaratibu  na kuyaeemea kwa nguvu zake zote matatizo sugu yanayowakabili Watanzania wanyonge kama maji, umeme na bei za mafuta,” amesema Hamad.

Maalim Seif aliteuliwa kuwa Mwenyekiti wa ACT-Wazalendo, Machi 2020, nafasi aliyohudumu hadi alipofariki dunia tarehe 17 Februari 2021.

error: Content is protected !!