Friday , 19 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa CCM yateta na viongozi wafanyabiashara Kariakoo
Habari za Siasa

CCM yateta na viongozi wafanyabiashara Kariakoo

Spread the love

 

CHAMA tawala nchini Tanzania- Chama Cha Mapinduzi (CCM ) kimesema, iwapo kila Mtanzania atawajibika na kufanya kazi kama yalivyo malengo, mipango na mikakati ya Rais Samia Suluhu Hassan, nchi hiyo itapaa na kuwa nchi yenye uchumi unaojitegemea. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Kimesema uamuzi wa Serikali ya awamu ya sita kuendeleza kaulimbiu ya ‘kazi iendelee’ ni kumtaka kila mtu anayeishi mjini na kijijini atambue wajibu wa kujituma, kufanya kazi, kuzalisha mali na kuitumikia nchi yake.

Hayo yalielezwa jana Jumanne, tarehe 30 Novemba 2021 na Katibu wa Halamshauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka alipokutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa jumuiya ya wafanyabiashara wa Karikoo, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.

Wafanyaboashara hao, walifika ofisini hapo kwa ajili ya kujitambulisha baada uchaguzi wa kuwapata viongozi wapya.

“Siku moja ikitoke Watanzania tukayaelewa malengo ya kisera na kimkakati ya serikali ya awamu ya sita, yanayotaka watu kujituma, ndipo tutakapoondokana na kadhia ya umasikini. Binadamu anapoamini kufanya kazi ni kama adhabu au utumwa huo ni mtazamo hasi usiofaa kufuatwa,” alisema Shaka.

Alisema katika kipindi kifupi cha uongozi wa Rais Samia ameakisi mambo yaliyokuwa yakitamaniwa na jamii yatokee, sauti ya Rais Samia imetoa mwangwi ili kuwazindua waliotaka kukata tamaa ambapo fikra, akili na mioyo ya Watanzania imepata ratiba mpya kwa kuzingatia mambo ya msingi yanayotamaniwa na kutoa uamuzi wa haki.

“Tulipopata uhuru na kufuzu Mapinduzi ya Zanzibar, kaulimbiu za marais na waasisi wa taifa, marehemu Mwalimu Julius Nyerere na Hayati Mzee Abeid Amani Karume, ilimtaka kila mtu afanye kazi. Ikaelezwa kazi ni kipimo na thamani ya utu wa mtu.”

“Tafsiri ya uhuru ni kufanya kazi. Watu walishiriki kwa pamoja kufanya za maendeleo, leo hii Rais Samia anaendeleza maono ya waasisi wetu hasa katika suala la uchumi wa kipato kwa Watanzani,” alisema

Shaka alisema, CCM inaridhishwa jinsi wananchi wanavyofanya shuhuli zao za uzalishaji na kuipongeza Serikali ya Rais Samia kwa kuendelea kuboresha huduma za kijamii na miundombinu ya kiuchumi ili kuharakisha maendeleo katika kukuza uchumi wa nchi kukiwa na amani na utulivu.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika kikao hicho, viongozi wa jumuiya hiyo walisema kilichowapeleka hapo ni kuimarisha ushirikiano, kwa kuwa CCM ndicho chama chenye ilani inayotekelezwa na serikali.

Walisema wanaamini, Serikali ya Rais Samia, imejipambanua kutaka kukuza wafanyabiashara wa ndani, tunaamini iwapo tutaendelea kuwa karibu, hata zinapotokea changamoto mbalimbali tunaweza kuzitafutia ufumbuzi mapema kabla ya kuyumbusha biashara zetu na uwekezaji kwa ujumla.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Tanzania, Uturuki zanuia kukuza biashara, uwekezaji

Spread the loveSERIKALI za Tanzania na Uturuki zimekubaliana kuendeleza dhamira ya kuimarisha...

Habari za Siasa

Tume huru ya uchaguzi yatangaza ajira watendaji daftari wapiga kura

Spread the love  TUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC), imetangaza nafasi...

Habari za SiasaTangulizi

Chadema yatangaza ruti awamu ya pili maandamano

Spread the love  CHAMA cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kimesema awamu ya...

Habari za Siasa

CCM yamkana mwenyekiti UVCCM aliyetaka wapinzani wapotezwe

Spread the love  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimejitenga na kauli ya mwenyekiti...

error: Content is protected !!