Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa ya Ofisi ya Raia (TAMISEMI), imeliomba Bunge kuwaidhinishia bajeti yake kwa mwaka wa fedha wa 2022/23, inayogharimu kiasi cha Sh. trilioni 8.77. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).
Ombi hilo limetolewa leo Alhamisi, tarehe 14 Aprili 2022 na Waziri wa TAMISEMI, Innocent Bashungwa, akiwasilisha makadrio ya mapato na matumizi kwa mwaka huo wa fedha, bungeni jijini Dodoma.
“Naomba Bunge lako tukufu likubali kuidhinisha makadirio ya mapato na matumizi kwa mwaka wa fedha wa 2022/23, ya jumla ya Sh. 8.778, kwa ajili ya Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Tume ya Utumishi wa Walimu na mikoa inayojumuisha halmashauri 184,” amesema Bashungwa.
Bashungwa amesema, kati ya fedha hizo, Sh. 5.511 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida yanayojumusiha mishahara na Sh. 4.626 trilioni na Sh. 884.861 bilioni ni za matumizi mengineyo, huku Sh. 3.267 trilioni zikiwa za miradi ya maendeleo.
Leave a comment