Friday , 26 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Simbachawene azindua kongamano msaada wa kisheria
Habari Mchanganyiko

Simbachawene azindua kongamano msaada wa kisheria

Spread the love

WAZIRI wa Katiba na Sheria, George Simbachawene amezindua kongamano la msaada wa kisheria la 2022, pamoja na Ripoti ya Wadau wa Upatikanaji wa Haki nchini Tanzania, iliyoandaliwa na Shirika la Legal Services Facility (LSF). Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma…(endelea).

Uzinduzi huo umefanyika leo tarehe 31 Machi 2022, jijini Dodoma na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wa sekta ya msaada wa kisheria.

Simbachawene amesema kongamano hilo linalofanyika kwa siku mbili, kuanzia jana hadi leo Alhamisi, tarehe 31 Machi 2022, limewaleta pamoja wadau wa sekta ya msaada wa kisheria kwa ajili ya kuangalia namna ya kuboresha sekta hiyo.

Pia, Simbachawene amesema kongamano litaisadia Serikali kupata maoni ya wadau kuhusu Sheria ya Msaada wa Kisheria ya Mwaka 2017.

“Kabla ya kutungwa na kupitishwa kwa Sheria ya Msaada wa Kisheria ya Mwaka 2017, wadau wa sekta hii hasa watoa huduma za msaada wa kisheria na wasaidizi wa kisheria, walikuwa wakikumbana na changamoto nyingi kubwa ikiwemo kutokutambuliwa katika taasisi mbalimbali za mifumo ya utoaji haki,” amesema Simbachawene.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu LSF, Lulu Ng’wanakilala, amesema kongamano hilo ni sehemu kubwa ya mafanikio ambayo shirika lake linajivunia kwa kushirikiana na wadau wengine, hasa Serikali katika kuwezesha upatikanaji wa haki.

“Tangu mwanzo LSF imekuwa mdau mkuu wa serikali katika kuhakikisha tunaendelea kufanya kazi kwa karibu kuwezesha upatikanaji wa haki, ikiwemo kuchangia katika kuwezesha sheria ya msaada wa kisheria nchini Tanzania inapatikana. LSF kama shirika lisilo la kiserikali tumekuwa tukifanya kazi ya kukuza upatikanaji wa haki kupitia uwezeshaji wa kisheria,” amesema Ng’wanakilala na kuongeza:

“Uwepo wa sheria hii umekuwa nyenzo muhimu kwetu, katika kuongeza upatikanaji wa haki kupitia wadau wetu wakubwa ambao wamekuwa wakitoa huduma za msaada wa kisheria na wasaidizi wa kisheria, kwa watu wote hasa wanawake na wasichana.”

 

Naye Msajili wa Msaada wa Kisheria, Felistas Mushi amesema kuwa katika kipindi cha miaka mitano changamoto kubwa imekuwa ada ya usajili wa wasaidizi wa kisheria lakini hata hivyo serikali imeamua kufuta ada hiyo ili kuruhusu wasaidizi wa kisheria kujisajili kwa wingi zaidi.

“Mpaka sasa tuna wasaidizi wa kisheria 757 ambao wamejisajili katika mfumo wa serikali kama watoa huduma za mnsaada wa kisheria. Vilevile tuna mashirika 202 tu ya wasaidizi wa kisheria yaliyosajiliwa baada ya kukidhi vigezo. Kuanzia mwaka mwezi wa pili ada hizo ambazo zilionekana ni kikwazo zimefutwa kabisa,” amesema Mushi.

Meneja Programu wa LSF, Deogratias Bwire akizungumzia ripoti ya wadau wa upatikanaji haki, amesema kuna zaidi ya wadau 30 kwenye sekta ya msaada wa kisheria, ambao wana umuhimu katika kuhakikisha haki za wananchi zinafikiwa.

“LSF tumefanya utafiti na kuja na ripoti hii muhimu kwa wadau wa upatikanaji wa haki nchini, ripoti imebainisha miongoni mwa wa wadau wakubwa katika utoaji huduma za msaada wa kisheri, a ni wasaidizi wa kisheria, mahakama, polisi, viongozi wa serikali, viongozi wa dini,” amesema Bwire na kuongeza:

“Bila kusahau viongozi wa kimila. Ripoti hii inaonyesha kama wadau wote wataunganisha nguvu ya pamoja kuna uwezekano mkubwa wa kuboresha zaidi upatikanaji wa haki kwa wananchi.”

Ripoti hiyo imeandaliwa na LSF, chini ya ufadhili wa Taasisi ya Denmark ya Haki za Binadamu (The Danish Institute For Human Rights).

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!