December 1, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Simba yatumia dakika 3 kuwaua Wabotswana

Spread the love

 

DAKIKA tatu zimetosha kwa mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara 2020/21, Simba kuanza safari vyema ya michuano ya Klabu Bingwa Afrika kwa kuibuika na ushindi wa 2-0 dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea).

Mchezo huo wa awali, umechezwa leo Jumapili katika Uwanja wa Taifa wa Botswana ukishuhudia vijana hao wa Msimbazi jijini Dar es Salaam, wakitumia dakika tatu za kipindi cha kwanza kujinyakulia ushindi huo muhimu.

Alikuwa ni kiungo mkabaji raia wa Uganda, Thadeo Lwanga aliyeifungia Simba bao la kwanza dakika ya tatu kipindi cha kwanza, baada ya kutokea piga nikupige kwenye lango la Galaxy na yeye kupiga shuti kali.

Dakika tatu baadaye yaani dakika ya sita, nahodha wa kikosi hicho, John Bocco aliindikia Simba bao la pili kwa shuti kali na hadi dakika 90 zinamalizika, Simba wametoka kifua mbele.

Mchezo wa pili wa marudiano, utapigwa wiki moja baadaye katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, jijini Dar es Salaam. Ikiwa Simba itashida au kutoka sare mchezo huo, utawapeleka hatua ya makundi ya michuano hiyo.

Ili Galaxy iitoe Simba, itahitaji kushinda magoli 3-0 katika Uwanja wa Mkapa au 4-1.

error: Content is protected !!