Friday , 2 June 2023
Home Kitengo Michezo Simba yaendeleza vipigo, Azam yapaa kileleni
Michezo

Simba yaendeleza vipigo, Azam yapaa kileleni

Spread the love

MABIGWA watetezi wa Ligi Kuu ya Vidacom Tanzania Bara 2020/21, Simba imeendelea kutoa vipigo baada ya kuofunga Gwambina FC 3-0. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Simba imeibuka na ushindi huo wa pili mfululizo katika mchezo uliochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam na kuwafanya kufikisha pointi 10 katika michezo minne.

Katika mchezo huo, Simba iliwalazimu kusubiri hadi dakika ya 40 ya kipindi cha kwanza kujipatia goli lililofungwa na Meddie Kagere kwa kichwa akiunganisba mpira wa kona uliopigwa na Lous Miquesson.

Hadi timu hizo zinakwenda mapumziko, Simba ilikuwa mbele kwa goli hilo.

Kipindi cha pili kilipoanza, beki kisiki wa mabingwa hao, Pascal Wawa aliindikia Simba goli dakika ya 50 baada ya kuachia mkwaju nje ya 18 na kuwafanya Simba kufikisha 2-0.

Super sub, Chris Mgula akiingia dakika ya 75 ya mchezo, akionekana kutoendeleza wimbi lake la kufumania nyavu, dakika ya 93 aliiandikia Simba goli la 3 akiunganisha basi safi iliyopigwa na Bernard Morrison.

Baada ya kucheza mechi mbili mfululizo kwenye dimba la Mkapa, mchezo unaofuata tarehe 4 Oktoba 2020 Simba itawafuata JKT Tanzania jijini Dodoma kwenye Uwania wa Jamhuri.

Nahodha wa Gwambina, Jacob Massawe amesema,”Tunawapongeza Simba kwa matokeo ya leo. Wametengeneza nafasi nyingi na tunakubali kwa ushindi wao.”

“Mpira ni mchezo wa makosa, ukikosea mwenzao anayatumia na walimu na benchi letu wameona makosa na imani yangu, tutafanya vizuri sana,” amesema Massawe

Naye Nahodha Msaidizi wa Simba, Mohamed Hussein amesema,”Mchezo ulikuwa mgumu hasa kipindi cha kwanza. Baada ya kupata goli lile na kwenda mapumziko, mwalimu alitupa maelekezo ambayo tukayafanyia kazi.”

Hussein amesema, Gwambina ni timu nzuri na inaonekana wanafuata maelekezo.

Katika michezo ya awali, Azam FC iliibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons, mchezo uliochezwa Uwanja wa Nelson Mandela, Sumbawanga Mkoa wa Rukwa.

Ushindi huo wa nne mfululizo kwa Azam umewafanya kufikisha pointi 12 na kuongoza msimamo wa ligi hiyo ambayo imefikia raundi ya nne.

Katika mchezo wa kwanza uliochezwa saa 8:00 mchana kwenye Uwanja wa Ushirika-Moshi mkoani Kilimanjaro, ulishuhudia Polisi Tanzania ikitoa kipigo cha 3-0 kwa Dodoma Jiji.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Dk. Mkwizu: Afrika tudumishe utamaduni

Spread the love  MWENYEKITI wa Jumuiya ya Tawala za Mitaa Mkoa wa...

Michezo

‘EONII’ kuteka tasnia ya filamu

Spread the love  UZINDUZI wa Filamu ya Kisayansi ya ‘EONII’ uliofanyika Mei...

Michezo

NBC Dodoma Marathon yazinduliwa, wakiambiaji 6,000 kushiriki

Spread the loveBENKI ya NBC imetangaza kufanyika kwa mbio kubwa za NBC...

Michezo

Rais Samia anunua tiketi 5000 Yanga vs USM Alger

Spread the loveRAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu...

error: Content is protected !!