June 30, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simba haishikiki, yatwaa tena kombe mbele ya Yanga

Spread the love

BAO la dakika ya 79, lilofungwa na Thadeo Lwanga, lillitosha kuifanya Simba kutetea ubingwa wake wa kombe la Shirikisho (ASFC), dhidi ya Yanga, kwenye mchezo uliopigwa kwenye dimba la Lake Tanganyika mkoni Kigoma. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Mchezo huo ambao uliudhuriwa na idadi kubwa ya mshabiki, ulianza kupigwa majira ya saa 10 kamili jioni.

Mchezo huo ulianza kwa timu zote kushambuliana kwa zamu kwenye kipindi cha kwanza na ulikuja kubadilika kwenye dakika ya 45+2, mara baada ya kiungo wa klabu ya Yanga, Mukoko Tunombe kuoneshewa kadi nyekundu kufuatia kupiga kiwiko nahodha wa Simba John Bocco.

Mpira huo ulikwenda mapumziko huku timu hizo zikiwa hazijafungana.

Kipindi cha pili kilipo rejea kocha wa klabu ya Simba Didie Gomes, huku akijua Yanga wapo pungufu alifanya mabadiliko kwa kumuingiza Bernard Morrison na kumpumzisha Larry Bwalya.

Bao la Simba lilipatikana kwa njia ya kona, mara baada ya Lwanga kiungo wa Simba kuunganisha mpira kwa kichwa uliopigwa na Luis Miquison.

error: Content is protected !!