Sunday , 5 February 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Dk. Hoseah  ajitosa sakata la Mbowe kukamatwa, TLS kutoa msimamo
Habari za Siasa

Dk. Hoseah  ajitosa sakata la Mbowe kukamatwa, TLS kutoa msimamo

Dk Edward Hoseah, Rais wa TLS
Spread the love

 

RAIS wa Chama cha Wanasheria wa Tanganyika (TLS), Dk. Edward Hoseah, ameiomba Serikali imfikishe mahakamani au imuache huru, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), anayeshikiliwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za ugaidi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Wito huo umetolewa leo tarehe 25 Julai 2021 na Dk. Hoseah, siku nne baada ya Mbowe kukamatwa akiwa katika Hoteli ya Kingdom jijini Mwanza, usiku wa kuamkia tarehe 21 Julai mwaka huu, akijiandaa kushiriki kongamano la kudai katiba mpya, lililoandaliwa na Chadema.

Baada ya kukamatwa na wenzie 14 jijini Mwanza, Mbowe alisafirishwa kuelekea Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, alikohojiwa kuhusu tuhuma za ugaidi. Wenzake wameachwa huru jana tarehe 24 Julai 2021 na Jeshi la Polisi Mwanza.

Akizungumzia tukio hilo, Dk. Hoseah amedai kwamba kitendo cha mamlaka kumshikilia Mbowe pasina kumfikisha mahakani au kumuacha huru, ni kukiuka sheria za nchi.

“Ikiwa kuna tuhuma nyingine dhidi yake, bado kwa sheria zetu alipaswa kuwa amefikishwa kwenye mamlaka za kisheria  na si kuendelea kuzuiliwa. Natoa wito kwa mamlaka kumwachia huru, kwa sababu kuendelea kumshikilia ni kukiuka utaratibu uliowekwa kwa mujibu wa Sheria,” amedai Dk. Hoseah.

Aidha, Dk. Hoseah amesema TLS inafuatilia kwa ukaribu tukio hilo, kisha itatoa msimamo wake.

“Chama cha Mawakili wa Tanganyika, tunaendelea kufuatilia kwa ukaribu suala hili na tutatoa msimamo wetu na mwelekeo baada ya mashauriano kufanyika, kupitia Baraza la Uongozi la TLS, ” amesema Dk. Hoseah.

Kuhusu hatua ya Jeshi la Polisi kukamata wafuasi wa Chadema waliopanga kufanya kongamano jijini Mwanza, Dk. Hoseah amesema”kufanya kongamano haijawahi kuwa kosa la jinai kwa mujibu wa Katiba na Sheria za nchi. Katiba yetu ibara ya 21(1) inatoa haki ya kujumuika na ibara ya 13(1) inatoa masharti ya watu wote kuwa sawa mbele ya Sheria.”

“Kitendo cha kumkamata usiku wa manane  Mbowe na wenzake, kwa sababu ya kuandaa kongamano ni ukiukwaji wa Katiba na Sheria za nchi yetu,” amedai Dk. Hoseah.

Baada ya Mbowe na wenzake kukamatwa, makundi mbalimbali, ikiwemo vyama vya siasa vya upinzani nchini Tanzania na jumuiya za kimataifa, yalipinga tukio hilo na kutaka mamlaka husika ziwaache huru.

Hata hivyo, Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa, alitoa wito kwa makundi hayo, kuliacha Jeshi la Polisi lifanye kazi yake, kisha litatoa taarifa rasmi juu ya tukio la Mbowe kukamatwa.

3 Comments

  • Heko TLS kwa msimamo wa kutetea sheria na katiba ya nchi. Wengine mbona kimya? Wakuu wa dini? Asasi za kiraia? Vyombo vya habari? JITOKEZENI! Leo kwa Mbowe kesho kwenu

  • Kuna udikteta wa aina mbili… udikteta wa mtu dhidi ya watu na udikteta wa chama dhidi ya vyama. Tangu “Chama kushika hatamu” imekuwa kawaida kwa ukamataji wa kisiasa kupewa sura ya jinai.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Prof. Muhongo aungana na wananchi ujenzi maabara za sekondari

Spread the loveMBUNGE wa Musoma Vijijini, Profesa Sospeter Muhongo, kwa kushirikiana na...

Habari za Siasa

CCM apiga marufuku wazazi kuwatumia watoto wa kike kwenye mambo ya kimila

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Taifa Daniel Chongolo...

Habari za Siasa

Ofisi za mabalozi wa mashina zitumike kuwale vijana kimaadili – Chongolo

Spread the loveKATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Daniel Chongolo ameagiza...

Habari za Siasa

Vijana ACT-Wazalendo Dar wampa tano Rais Samia

Spread the love  NGOME ya Vijana ya Chama cha ACT-Wazalendo, kimempongeza Rais...

error: Content is protected !!