December 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Serikali yatoa Bil 688 mradi wa umeme Rufiji

Spread the love

SERIKALI imetoa kiasi cha Shilingi 688.6 bilioni, kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa umeme katika maporomoko ya Mto Rufiji. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Dotto James, Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango leo tarehe 24 Aprili 2019, amekabidhi hundi ya kiasi hicho cha fedha kwa mkandarasi anayejenga mradi huo, Kampuni ya Arab Contractors ya nchini Misri, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza baada ya kukabidhi hundi hiyo James amesema, malipo hayo ni sehemu ya kwanza na kwamba yamegawanyika katika sehemu mbili.

“Malipo haya ya awali yataenda sambamba na malipo mengine ambapo jumla take itakuwa shillingi tilioni 1 kwa ujumla” amesema James.

Naye  Msemaji Mkuu wa Serikali, Dk. Hassan Abbas kupitia taarifa yake aliyoitoa katika ukurasa wake wa Twitter, amesema lengo la serikali la kutoa fedha hizo ni kuhakikisha kwamba hali ya upatikanaji wa nishati ya umeme inaimarika kwa ajili ya kusaidia kukuza kasi ya uchumi wa viwanda kwa ajili ya kubadili maisha ya Watanzania.

“Serikali yatoa mabilioni kuanza utekelezaji wa mradi wa Umeme wa Maji Rufiji, lengo ni kuihakikishia nchi umeme wa kutosha, kusaidia kasi ya uchumi wa viwanda na kuyabadili maisha ya Mtanzania mmoja mmoja,” inaeleza taarifa hiyo ya  Dk. Abbas.

error: Content is protected !!