Saturday , 2 December 2023
Home Habari Mchanganyiko Madaktari Muhimbili wahaha kumuokoa Mariam
Habari MchanganyikoTangulizi

Madaktari Muhimbili wahaha kumuokoa Mariam

Spread the love

MARIAM Rajab Mimbe (25), anayesumbuliwa na kidonda kikubwa kwenye mgongo, upande wake wa kulia, anaendelea vizuri na sasa yuko njiani kuelekea katika hospitali ya Ocean Road, jijini Dar es Salaam. Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Mariam ambaye amelezwa katika hosiptali ya taifa ya Muhimbili (MNH), amepatwa na maradhi hayo, takribani miaka 10 iliyopita.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, leo tarehe 24 Aprili, daktari bingwa wa upasuaji katika hospitali hiyo, Ibrahim Mkoma amesema, tayari wamebaini ugonjwa unaomsumbua Mariam.

“Tayari tumegundua maradhi yanayomsumbua Mariam. Tumemfanyia uchunguzi na kesho Jumatano, atahamishiwa hospitali ya Ocean Road ili kuanza matibabu rasmi,” ameeleza.

Hata hivyo, Dk. Mkoma amegoma kutaja ugonjwa unaomsumbua Mariam, ingawa wengi wa wagonjwa wanaopelekwa katika hospitali ya Ocean Road, husumbuliwa na maradhi ya kansa.

Amesema, “…kulingana na maadili yetu ya kazi, ugonjwa ni siri kati ya mgonjwa na daktari wake. Lakini tumechukua vipimo mbalimbali vya damu na tumekwenda maabara ili kubaini aina ya ugonjwa wake.”

Mariam alifikishwa Muhimbili wiki iliyopita, akitokea kijijini kwao, Mnung’una, mkoani Singida.

Alipokelewa katika idara ya magonjwa ya dharura na mara moja akaanza kufanyiwa vipimo  na kupatiwa matibabu yenye lengo la kupunguza maumivu ya kidonda kinachomsumbua.

Dk. Mkoma amesema, wamejua namna ya kumtibu Mariam na kwamba, baada ya kumaliza matibabu yake katika hospitali ya Ocean Road, atarejeshwa Muhimbili kwa uchunguzi zaidi na kufuatilia afya kwa karibu afya yake.

Dk. Mkoma amesema, Mariam amefanyiwa vipimo kadhaa ili kubaini ugonjwa unaomsumbua, ikiwamo CT Scan kwa upande wa kichwa na kifua.

Kwa upande wake, Mariam ameushukuru uongozi wa hospitali ya Muhimbili na serikali kwa ujumla kwa kumpatia matibabu.

Aidha, amewashukuru wananchi wote walioguswa na ugonjwa wake na hivyo kufuatilia kuanzia alipokuwa Singida hadi alipofika Muhimbili na wengine kumsaidia na kumuombea.

“Nawashukuru wote walioniombea na kunitakia afya njema. Sina ninaloweza kuwalipa, bali Mungu atawalipa. Natokea familia ya kimasikini; wazazi wangu hawana uwezo wa kunisaidia tatizo linalonikabili,” alisema Mariam kwa sauti ya masikitiko.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

AfyaHabari Mchanganyiko

GGML waungana na Biteko kuanika mbinu za mapambano dhidi ya Ukimwi

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto Biteko...

Habari MchanganyikoTangulizi

Mwalimu jela miaka mitatu kwa rushwa

Spread the loveMAHAKAMA ya Hakimu Mfawidhi, wilaya ya Igunga, mkoani Tabora imemhukumu...

Habari Mchanganyiko

Waziri Bashungwa aagiza wahandisi kujengewa uwezo

Spread the loveWAZIRI wa Ujenzi, Innocent Bashungwa ameiagiza Bodi ya Usajili wa...

Habari Mchanganyiko

Heche ataka mawakili vijana kuamka sakata Mpoki

Spread the loveMWENYEKITI wa Mawakili Vijana Tanzania kutoka Chama cha Mawakili wa...

error: Content is protected !!