Sunday , 19 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Samia kufanya ziara ya siku 4 Kigoma
Habari Mchanganyiko

Samia kufanya ziara ya siku 4 Kigoma

Spread the love

RAIS Samia Suluhu Hassan anatarajiwa kufanya ziara ya kikazi ya siku nne mkoani Kigoma, kuanzia tarehe 16 hadi 19, Oktoba mwaka huu. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari kuhusu ziara hiyo, leo tarehe 11 Oktoba, 2022 Mkuu wa mkoa wa Kigoma, Thobias Andengenye amesema ziara ya Rais Samia itaanzia wilayani Kakonko.

Amesema akiwa mkoani Kigoma, pamoja na mambo mengine Rais Samia atafungua, kuzindua na kuweka mawe ya msingi katika miradi mbalimbali ya maendeleo.

Aidha, Andengenye amewataka wakazi wa wilaya za mkoa wa Kigoma ambazo Rais atapitia zikiwemo za Kakonko, Kibondo Kasulu, Buhigwe na Kigoma kujitokeza kwa wingi kumpokea kiongozi huyo.

Ziara ya Rais Samia Suluhu Hassan mkoani Kigoma ni ya kwanza tangu aingie madarakani mwezi Machi mwaka 2021.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

CCM yamteua Pele kuwa mgombea ubunge Kwahani

Spread the loveKamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM)...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Canada yatenga bilioni 38 kutekeleza mradi ya kuinua vijana TZ

Spread the loveSERIKALI ya Canada kupitia ‘CARE International Canada’ imetenga takribani Sh...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Ujenzi kituo cha kupoza umeme Chalinze wafikia asilimia 93.7

Spread the loveKamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini imeeleza...

Habari Mchanganyiko

Balile ateuliwa rais wa wahariri Afrika Mashariki

Spread the loveJumuiya ya Wahariri wa Afrika Mashariki (EAES), imemchagua Mwenyekiti wa...

error: Content is protected !!