NAHODHA wa timu ya Taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ Mbwana Samatta anayekipiga kwenye klabu ya Astorn Villa huenda akauzwa katika dirisha hili kubwa la usajili kufuatia uongozi wa klabu hiyo kumsajili Ollie Watkins kutoka klabu ya Brentford. Anaripoti Kelvin Mwaipungu … (endelea).
Samatta mwenye umri wa miaka 27, alijiunga na Astorn Villa kwenye dirisha dogo la usajili mwezi Januari akitokea klabu ya Genk inayoshiriki Ligi Kuu nchini Ubelgiji.
Baadhi ya vyombo vya habari kutoka nchini Uingereza vimeripoti kuwa Samatta ni moja ya wachezaji watakaondoka kwenye klabu kabla ya dirisha la usajili kufungwa 4 Oktoba, 2020 licha ya kudumu kwa miezi nane.
Taarifa zinaeleza kuwa huenda mshambuliaji huyo akatimkia kwenye klabu ya Besiktas inayoshiriki Ligi Kuu nchini Uturuki ambayo imeonesha nia ya kuhitaji huduma ya mshambuliaji huyo.