Tuesday , 30 May 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Lissu atikiswa, chopa yake yagomewa
Habari za SiasaTangulizi

Lissu atikiswa, chopa yake yagomewa

Spread the love

HELKOPTA (chopa) iliyotarajiwa kumbeba Tundu Lissu, mgombea urais kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), kuelekea Bagamoyo mkoani Pwani, imegomewa kuruka. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Taarifa kutoka Chadema zinaeleza, Lissu na timu yake ya kampeni, walikuwa kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Malimu Julius Nyerere (JNIA), tayari kuingia kwenye chopa hiyo na kuanza safari ya kuelekea Bagamoyo ili kuendelea na kampeni.

Ratiba ya mikutano mitano ya kampeni za Lissu ilionesha kwamba, Lissu angekuwa na mkutano wa hadhara leo tarehe 10 Septemba 2020 Bagamoyo.

Taarifa ya Tumaini Makene, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya chama hicho imeeleza, kwamba Mamlaka ya Viwanja vya Ndege (TCAA), ndio iliyotoa barua ya kuzuia chopa hiyo kuruka. hata hivyo, hakueleza sababu zilizotolewa na TCAA.

“Taarifa za kukataliwa kwa helikopta hiyo kuruka, zilitolewa kwa Ofisa Mnadhimu wa Kampeni, Amani Golugwa wakati msafara wa Lissu ukielekea kupanda ndege baada ya kumaliza taratibu zote za ukaguzi wa kiusalama uwanjani,” imeeleza taarifa ya Makene.

Makene amesema, kutokana na katazo la TCAA, chama hicho kimelazimika kutafuta utaratibu mwingine wa kuweza kufanikisha safari ya Lissu kwenda kwenye mkutano huo. 

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Uamuzi juu ya wakurugenzi kusimamia uchaguzi 13 Juni

Spread the love  MAHAKAMA ya Afrika ya Haki za Binadamu (ACHPR), imepanga...

Habari MchanganyikoTangulizi

Jeshi la Polisi kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam katika utafiti

Spread the love  JESHI la Polisi Nchini limesema kuwa katika kukabiliana na...

KimataifaTangulizi

Mtuhumiwa wa mauaji ya halaiki ya Rwanda akamatwa Afrika Kusini

Spread the love  MMOJA wa watuhumiwa wakuu wa mauaji ya Kimbari ya...

Habari za Siasa

Musoma Vijijini waomba ujenzi wa barabara uanze haraka

Spread the loveJIMBO la Musoma Vijijini, mkoani Mara, limeomba Serikali kuhakikisha ujenzi...

error: Content is protected !!