Friday , 26 April 2024
Home Gazeti Habari za Siasa Sabaya, wenzake wapigwa miaka 30 jela
Habari za SiasaTangulizi

Sabaya, wenzake wapigwa miaka 30 jela

Lengai ole Sabaya
Spread the love

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha, imemhukumu kifungo cha miaka 30 jela, aliyekuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai, Mkoa wa Kilimanjaro, Lengai Ole Sabaya na wenzake wawili. Anaripoti Mwandishi Wetu, Arusha … (endelea).

Hukumu hiyo imetolewa baada ya mahakama hiyo, kumkuta na hatia katika kesi iliyokuwa ikimkabili ya unyang’anyi wa kutumia silaha yeye pamoja na wenzake, Sylvester Nyegu na Daniel Mbura

Hukumu hiyo imetolewa leo Ijumaa, tarehe 15 Oktoba 2021 na Hakimu Mkazi Mwandamizi, Odira Amworo.

Hakimu Mwandamizi Amworo amesema, mahakama imethibitisha pasi na shaka Sabaya alitenda makosa hayo.

Kabla ya kutoa adhabu, Hakimu Odira alimpa fursa Sabaya ya kusema chochote ambapo aliiomba mahakama imuonee huruma kwani siyo yeye bali alikuwa anatekeleza maagizo ya mamlaka yake ya uteuzi na ana mchumba ambaye walikuwa wafunge ndoa kwani mahari amekwisha lipa.

Sabaya na wenzake walikuwa wanatuhumiwa kuvamia na kufanya unyang’anyi wa kutumia silaha wa zaidi ya Sh. 2.7 milioni, katika duka la Mohamed Saad, tarehe 9 Februari 2021.

Kesi hiyo, ilisikilizwa mfululizo kuanzia tarehe 19 Julai hadi 24 Agosti 2021 baada ya Sabaya na wenzake, kusomewa maelezo ya awali ya kesi hiyo mhakamani hapo, tarehe 16 Julai 2021.

Aidha, tarehe 24 Agosti 2021 Hakimu Mkazi Mwandamizi, Odira Amworo alipanga tarehe 1 Oktoba kuwa siku ya hukumu baada ya mahakama hiyo kumaliza kusikiliza ushahidi wa pande zote mbili. Hata hivyo, iliahirishwa kutolewa hadi leo Ijumaa.

Sabaya na wenzake alifikishwa mahakamani baada ya Rais Samia Suluhu Hassan kutangaza kumsimamisha kazi tarehe 13 Mei 2021 ili kupisha uchunguzi wa tuhuma mbalimbali zilizokuwa zinamkabili.

Sabaya aliyewahi kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Mkoa wa Arusha, alianza safari ya kuwa mkuu wa wilaya ya Hai, tarehe 28 Julai 2018 baada ya aliyekuwa Rais wa Tanzania, Hayati John Magufuli, kumteua kuwa Mkuu wa Wilaya ya Hai.

1 Comment

  • MWANA WA KULITAFUTA MWANA WA KULI GET,ACHA AENDE AKAKUTANE NA WANAUME WASHOKA ALIOKUWA AKIWADHALILISHA KUTOKANA NA CHEO CHAKE UONGOZI NA NGAZI KUNA KUPANDA NA KUSHUKA TUWE MAKINI, NEXT MAKONDA

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari za Siasa

Prof. Muhongo akomalia matumizi nishati jadidifu kuondoa uhaba wa umeme

Spread the love  MBUNGE wa Musoma Vijijini (CCM), Profesa Sospeter Muhongo, ameendelea...

Habari za Siasa

Kilosa yawa mfano wa kuigwa miradi ya Mwenge nchini

Spread the love  KIONGOZI wa Mbio za Mwenge Kitaifa Godfrey Mzava amezitaka...

Habari za SiasaTangulizi

Biteko ataja vipaumbele 7 bajeti nishati 2024/25

Spread the love  NAIBU Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dk. Doto...

error: Content is protected !!