Friday , 26 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Rais Samia: Mkeka wa Ma-DC, DED, DAS waja
Habari Mchanganyiko

Rais Samia: Mkeka wa Ma-DC, DED, DAS waja

Spread the love
RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amesema hivi karibuni atafanya mabadiliko ya viongozi wa wilaya nchini. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mwanza…(endelea).
Viongozi hao ni Wakuu wa Wilaya (DC), Wakurugenzi (DED) na Makatibu Tawala (DAS).
Rais Samia alitoa taarifa hiyo jana Jumanne, tarehe 15 Juni 2021, akizungumza na vijana wa Tanzania, jijini Mwanza.
Akizungumza katika mkutano huo, Rais Samia alisema mkeka wa mabadiliko ya viongozi hao, utatoka hivi karibuni, baada ya mkeka wa Makatibu Tawala wa Mikoa (RAS), kutoka.
Kiongozi huyo wa Tanzania,  alifanya mabadiliko ya Ma-RAS, tarehe 30 Mei 2021, kwa kuteua wapya 11 na kuwahamisha tisa,  huku sita wakibaki katika mikoa yao.
“Karibuni nimeteua Ma-RAS,  kuna mkeka wa Ma-DC utakaotoka karibuni. Mbali ya mkeka wa Ma-DC,  bado nina mkeka wa wakurugenzi na Ma-DAS haujatoka,” alisema Rais Samia.
Rais Samia alitoa wito kwa vijana nchini, kuchangamkia fursa hizo, huku akiwataka wasiwaangushe watu wanaowateua.
“Nataka kuwaambia wote ni vijana, kwa hiyo hizo ndizo  fursa mlizonazo vijana, ingawa baadhi yenu tunapowapa fursa hizi mnakwenda kufanya mnavyofanya na kutuangusha.  Ningeomba mnapopata fursa hii mkazitumikie kwa umakini,” amesema Rais Samia.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!