Sunday , 5 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko Masheikh wa Uamsho waachiwa
Habari MchanganyikoTangulizi

Masheikh wa Uamsho waachiwa

Spread the love

 

MASHEIKH wawili kati ya 51, wa Jumuiya ya Uamsho na Mihadhara ya Kiislamu Zanzibar, waliokuwa wanakabiliwa na makosa ya ugaidi kwenye Kesi ya Jinai Na. 121/, katika Mahakama Kuu ya Tanzania, Kanda ya Dar es Salaam, wameachwa huru. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam…(endelea).

Akizungumza na MwanaHALISI Online kwa simu, leo tarehe 16 Juni 2021, Msemaji wa Shura ya Maimamu Tanzania, Ibrahim Mkondo, amesema Sheikh Mselemu Ally na Farid Ally Hadi, wameachwa huru kutoka katika mahakabusu ya Ukonga jijini Dar es Salaam, usiku wa jana tarehe 15 Juni 2021.

Hatua hiyo ya Masheikh kuachwa huru, imekuja takribani siku tatu tangu Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP), Sylvester Mwakitalu, kuzungumza na masheikh hao tarehe 12 Juni mwaka huu.

Mkondo amesema, Masheikh hao walisafirishwa kwa ndege usiku wa jana, kutoka katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, jijini Dar es Salaam, hadi visiwani Zanzibar.

Alipoulizwa sababu za Msheikh hao kuachwa huru huku kesi yao ikiendelea, Mkondo amesema hadi sasa haijafahamika sababu zake na kwamba shura hiyo imemtuma mwakilishi wake visiwani Zanzibar, kuzungumza nao ili wajue kinaga ubaga wa hatua hiyo.

“Inaonekana wamefutiwa mashtaka japo hatujapata taarifa vizuri, tumetuma mtu sasa hivi yuko njiani kwenda Zanzibar kwa ajili ya kuzungumza kujua nini kimetokea mpaka wameachiwa,” amesema Mkondo na kuongeza:

“Sababu hata mawakili wao hawana taarifa kuhusu hilo. Ila tunachofahamu wameachiwa jana usiku majira ya saa tatu, walipelekwa Airport (uwanja wa ndege), kusafirishwa kwenda Zanzibar. Tumetoa taarifa kwa ufupi lakini muda si mrefu tutatoa taarifa zaidi.”

Masheikh hao walikuwa wanadaiwa kati ya Januari 2013 na Juni 2014, walijihusisha na makosa ya ugaidi, kinyume na kifungu cha 27 (c), cha Sheria ya Kuzuia Ugaidi ya mwaka 2002.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Haya hapa majina 12 ya familia moja waliofariki kwenye ajali Tanga

Spread the love  MAJINA 12 kati ya 17 ya waliofariki dunia katika...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia awalilia 17 waliofariki ajalini wakisafirisha maiti

Spread the love  RAIS Samia Suluhu Hassan, ametuma salamu za rambirambi kwa...

Habari Mchanganyiko

Wanawake wachimbaji wajenga zahanati kuokoa afya za wakazi 2000

Spread the love  ZAIDI wakazi 2,000 wa kijiji cha Nyamishiga Kata ya...

Habari Mchanganyiko

Baada ya Congo DR, Somalia mbioni kujiunga na EAC

Spread the love  TAIFA la Somalia liko mbioni kuwa mwanachama rasmi wa...

error: Content is protected !!