Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Rais Samia ashiriki kumbukizi ya Karume Zanzibar
Habari Mchanganyiko

Rais Samia ashiriki kumbukizi ya Karume Zanzibar

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, pamoja na Rais wa Zanzibar, Dk. Hussein Mwinyi, wameshiriki kumbukizi ya miaka 50 ya kifo cha muasisi wa Serikali ya Mapinduzi visiwani humo, Hayati Abeid Aman Karume, kilichotokea tarehe 7 Aprili 1972 . Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Kumbukizi hiyo imefanyika leo Alhamisi, tarehe 7 Aprili 2022, katika ofisi ndogo za CCM Zanzibar na kuhudhuriwa na viongozi wengine wa kitaifa, akiwemo Makamu wa Rais wa Tanzania, Dk. Phillip Mpango na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa.

Wengine waliohudhuria kumbukizi hiyo ni, Rais Mstaafu wa Zanzibar na mtoto wa hayati Karume, Amani Abeid Karume, pamoja na mama yake, Fatma Karume.

Makamu wa Rais wa visiwa hivyo, Othman Masoud Othman (wa kwanza) na Hemed Suleiman Abdullah (wa pili), Mufti Mkuu wa Zanzibar, Sheikh Saleh Omari Kabi, pamoja na Kaimu Kadhi Mkuu Zanzibar, Sheikh Hassan Othman Ngwali, ni miongoni mwa walioshiriki kumbukizi hiyo.

Katika kumbukizi hiyo, ilifanyika dua na fatha ya ufunguzi, iliyoendeshwa na Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, ambaye amemuomba Mungu amrehemu Hayati Karume pamoja na mashujaa wote waliotangulia mbele ya haki.

“Tunakuomba Mwenyezi Mungu usamehe mja wako huyo pamoja na mashujaa wote waliotanguliwa, waliyojitolea kwa ajili ya nchi hii yaZanzibar. Tunakuomba pia endelea kuwabariki viongozi wetu waweze kuwatumikia Watanzania kwa namna ambayo wewe unaipenda na kuiridhia,” amesema Sheikh Salum.

Baada ya Sheikh Salum kusoma dua hiyo, ilisomwa Quran tukufu na Al Ustaadhi, Abdulrahim Twalib Abdallah, kutoka Jumuiya ya Wasomaji Tajweed Zanzibar.

Rais wa Zanzibar, Dk. Mwinyi aliongoza kisomo cha Quran na kuhitimishwa na Sheikh Salum Juma Faki.

Naye Mjumbe wa Baraza la Ulamaa, Sheikh Hamis Abdulhamid, alitoa mawaidha katika kumbukizi hiyo, akisema Hayati Karume aliwawekea Wazanzibar msingi wa taaluma kwa kufungua Chuo cha Kiislamu 1972,ambacho kimetoa maulamaa, akiwemo yeye.

“Ametuwekea misingi hii sababu ije imfae kesho akhera na itamfaa sababu Mtume anatuhadithia kwamba mwanadamu anaacha mambo matatu ambayo ni muhimu sana, akasema ukifanya sadaka ambayo itaendelea na itawafaa wa baadaye, basi na yeye huko aliko atakuwa anapata fungu lake,” amesema Sheikh Hamis.

Sheikh Hamis, amewataka Wazanzibar na Watanzania kwa ujumla, kutamka mema yanayofanywa na watu waliotangulia mbele ya haki, ili wapate rehema mbele za Mungu.

“Na Mtume anatuambia kuhusu huyu atakayekwenda ndani ya haki, yatajeni mazuri yake. Si vibaya kusema yaliyokuwa mazuri ya waliotutangulia. Kabla ya hii kama yako yaliyojitokeza mabaya hayo yafunike. Haina haja ya kuyasambaza hata kama yalikuwa siyo, bali yale mema ndiyo yatakayotangazwa,” amesema Sheikh Hamis.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!