August 9, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Urusi hatarini kuondolewa UNHRC

Spread the love

NCHI ya Urusi iko hatarini kuondolewa ujumbe katika Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa (UNHRC), kufuatia hatua yake ya kuivamia kijeshi Ukraine na kusababisha mauaji ya raia. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa…(endelea).

Kwa mujibu wa mtandao wa BBC, leo Alhamisi, tarehe 7 Aprili 2022, wanachama wa UN, wanatarajia kupiga kura ya kuamua kama Urusi inastahili kuondolewa UNHRC, kufuatia uvamizi wa kijeshi walioufanya Ukraine.

Katika mchakato wa huo, Urusi itaondolewa kama theluthi ya wajumbe wa UN watapiga kura ya ndiyo.

Azimio la kuitishwa kwa kura hiyo lilitolewa na nchi ya Marekani, kufuatia mauaji ya raia wa Ukraine, katika maeneo ya Bucha, kwenye Jimbo la Kyiv.

Urusi imepinga hatua hiyo ikidai ni ukiukwaji wa kanuni za UNHRC, utakaodhoofisha mfumo wa haki za binadamu wa baraza hilo.

Mkuu wa Urusi UN, Gennady Galitov, ameonya nchi watakaopiga kura hiyo, kuwa taifa lake litaihesabu kama adui yake.

“Kusimamishwa kwa haki ya Urusi kama mjumbe wa UNHRC, ni kudharau kanuni ya baraza, kuathiri ufanisi wake na kudhoofisha kabisa uaminifu, sio tu kwa haki za binadamu, lakini katika mfumo mzima wa hakiza binadamu wa UN,” amesema Gatilov.

Vita nchini Ukraine ilianza mwishoni mwa Februari 2022, baada ya Rais wa Urusi, Vladimir Putin, kutangaza operesheni ya kijeshi nchini humo, ikiwa ni hatua ya kuishinikiza iache mpango wake wa kutaka kujiunga na Jumuiya ya Kujihami (NATO).

Mbali na Urusi kutaka Ukraine isijiunge na NATO, pia Taifa hilo linaunga mkono hatua ya waasisi wa mikoa ya mashariki ya nchi hiyo, kujitangazia uhuru na kutaka kuwa dola huru.

error: Content is protected !!