May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia amlilia Teddy Mapunda

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amesema, ameomboleza kifo cha Teddy Mapunda, akisema nchi imepoteza mwanamke hodari na mchaka kazi. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam ... (endelea). 

Samia ametoa salamu hizo kupitia kurasa zake za kijamii, kufuatia kifo cha Teddy kilichotokea Jumanne ya tarehe 4 Mei 2021, katika Hospitali ya Aga Khan, Dar es Salaam.

Ni baada ya kuugua kwa muda mfupi, alipokuwa akishiriki chakula cha jioni na marafiki zake, katika Hotel ya Serena, jijini humo.

Rais Samia ameandika “Nimehuzunishwa na kifo cha Teddy Mapunda. Tumepoteza Mwanamke hodari, mchapakazi, mbunifu, mahiri na aliyedhibitisha kwa vitendo kuwa Wanawake wanaweza.”

“Nitamkumbuka kwa jinsi alivyojitoa kwa Chama na Serikali na alivyoipenda nchi yake. Mungu amweke mahali pema peponi, Amina.”

Enzi za uhai wake, Teddy alikuwa mwanamichezo na alikuwa mjumbe kwenye kamati ya hamasa ya Taifa Star.

Pia, alikuwa Mjumbe wa Bodi ya Baraza la Habari Tanzania (MCL), akiwa kama makamu mwenyekiti wa kamati ya fedha na utawala.

error: Content is protected !!