May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Man United wahamia kwa Harry Kane

Spread the love

 

Klabu ya Manchester United ya nchini England ipo tayari kutoa kiasi Euro 90 milioni sawa na shilingi 250.8 bilioni, kwa jili ya kunasa saini ya mshambuliaji wa klabu ya Tottenham Harry Kane kwenye dirisha kubea la usajili. Anaripoti Kelvin Mwaipungu…(endelea)

Endapo usajili huo utakamilia Kane atakuwa mchezaji aliyenunuliwa kwa pesa nyingi ndani ya kikosi cha Manchester United na kuvunja rekodi ya Paul Pogba aliyenunuliwa kwa kiasi cha Euro 89.3 sawa na shilingi 248 bilioni akitoka klabu ya Juventus ya itary mwaka 2016.

Mabosi wa Manchester United ambao ni familia ya Glazer wanataka kufanya usajili wa mshambuliaji huyo hatari kwa sasa ndani ya Ligi Kuu England ili kuwapooza mashabiki wa timu hiyo walioandamana Jumapili ya Wiki hii na kufanya mchezo wao dhidi ya Liverpool kuahilishwa. 

Matajili hao kwa sasa wanataka kumsajili mshambuliaji huyo ili kutimiza hitaji la kocha wao Ole Gunner Solskjaer.

Taarifa za mchezaji kuondoka kwenye klabu hiyo yenye makazi yake London ni mara baada ya kutoa kauli ya kwamba lengo lake kwa sasa kama mchezaji ni kushinda mataji na timu.

Kocha wa Manchester United Ole Gunner Solskjaer

Ikumbukwe Februari mwaka huu mshambuliaji wa zamani wa klabu hiyo Jamie Defoe alimshauli mshambuliaji huyo kuwa kama anataka mfungaji bora wa muda wote kwenye kikosi hiko anaweza kubakia hapo lakini kama anataka kushinda mataji hana budi kuondoka Totenham.

Kauli hiyo inatiwa nguvu kutokana na siku 10 nyuma Tottenham ilipoteza mchezo wa fainali ya kombe la Ligi mbele ya Manchester City mara baada kukubali kichapo cha bao 1-0.

Pia mshambuliaji huyo akiwa na Tottenham walipoteza tena mchezo wa fainali ya ligi ya Mabingwa barani Ulaya Juni Mosi 2019 kwa mabao 2-0.

Mshambuliaji huyo kwa msimu huu ndani ya Ligi Kuu England amepachika jumla ya mabao 21, katika michezo 31 aliyocheza huku akitoa pasi za mabao (assist) 13, mashuti yaliolenga lango (Shorts on Target) 46, pasi 816 na nafasi alizotengeneza ni 31.

Manchester United kwa sasa ipo kwenye hatua ya nusu fainali ya michuano ya kombe la Europa kwa kupata ushindi wa mabao 6-2 dhidi ya As Roma kwenye mchezo wa Kwanza uliofanyika Old Trafford

error: Content is protected !!