May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia amlilia Mhandisi Mfugale

Spread the love

 

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, ametoa salamu za rambirambi kufuatia kifo cha Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (Tanroads), Mhandisi Patrick Mfugale. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Mhandisi Mfugale, alifikwa na mauti jana Jumanne, saa 5:00 asubuhi, tarehe 29 Juni 2021, katika Hospitali ya Benjamin Mkapa, jijini Dodoma.

Hadi anafikwa na mauti, amehudumu nafasi ya mtendaji mkuu kwa zaidi ya miaka kumi, kuanzia tarehe 23 Mei 2011, akiwa amesimamia ujenzi wa barabara zaidi ya kilomita 1,400 na madaraka mbalimbali yakiwemo ya juu.

Katika ukurasa wake wa Twitter, Rais Samia ameandika “Nimesikitishwa na taarifa ya kifo cha Mhandisi Patrick Mfugale (Mtendaji Mkuu-TANROADS).”

“Nitaukumbuka mchango mkubwa katika ujenzi wa miundombinu yetu hasa barabara, madaraja, reli na umeme.”

“Pole kwa Familia na Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi. Mungu amweke mahali pema peponi, Amina.”

Awali, jana Jumanne usiku, taarifa iliyotolewa na Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi ilisema, taratibu za mazishi zitatangazwa baadae.

error: Content is protected !!