May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia aeleza Kamala alivyopata Corona, “mimi mzima”

Spread the love

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amefafanua kuwa baada ya kukutana Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris, alipokuwa kwenye ziara nchini humo, Kamala alipimwa na majibu kutoka kuwa hana maambukizi ya virusi vya Corona.

Amesema wiki moja baada ya kukutana na makamu huyo wa Rais, aligundulika kuambukizwa virusi hivyo vinavyosababisha ugonjwa wa Covid- 19 hii ikiwa ni baada ya kiongozi huyo wa Marekani kwenye ziara zake za kikazi. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Rais Samia ametoa kauli hiyo leo tarehe 3 Mei, 2022  jijini Arusha katika maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari duniani.

Ametolea mfano namna alivyochorwa kikatuni kuelezea kuwa amemuambukiza Virusi vya Corona Makamu wa Rais wa Marekani, Kamala Harris.

“Nimeona kwenye mitandao ya kijamii… Rais wenu kaenda kuonana na Makamu wa Rais wa Marekani, baada ya wiki yule bibi yupo positive COVID-19, mimi mzima!

“Mtanzania kaweka kikatuni katia mshale unatoka kwangu unakwenda kwa Kamala kwamba mimi nimempa COVID-19 lakini alipimwa baada ya mimi kuondoka yupo negative, kaenda ziara karudi ndio yupo positive, ulizeni… mnajiandikia tu, miye nina ngozi ngumu, andikeni,” amesema.

Rais Samia alielekea nchini Marekani Aprili 13 hadi 28 mwaka huu kwenda kuzindua filamu inayotangaza utalii wa Tanzania maarufu kama ‘Royal tour’

Aidha, ametoa wito kwa vyombo vya habari kuelimisha umma kuhusu matumizi bora ya mitandao ya kijamii hasa ikizingatiwa wapo wengine wanaitumia vibaya kwa kuweka picha na video zisizo na maadili.

error: Content is protected !!