Sunday , 5 February 2023
Home Gazeti Habari Mchanganyiko PPRA yafanya utafiti matumizi ya kikosi kazi katika miradi ya maendeleo
Habari Mchanganyiko

PPRA yafanya utafiti matumizi ya kikosi kazi katika miradi ya maendeleo

Bwawa la Umeme Rufiji
Spread the love

MAMLAKA ya Kudhibiti Ununuzi wa Umma nchni (PPRA) imeeleza kuwa utumiaji wa utaratibu wa kikosi kazi “ Force Account “katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ni njia inayofaa ikiwa itasimamiwa vyema. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).

Hayo yalibainishwa katika utafiti mdogo uliofanywa na Mamlaka, ili kuangalia ufanisi wa utumiaji wa kikosi kazi katika miradi ya maendeleo ya ujenzi inayoendelea nchini. Utafiti huo ulihusisha miradi 175 iliyofanywa kwa njia ya kikosi kazi.

Meneja Utafiti na Nyaraka wa Mamlaka, Mhandisi Nashon Masunya alieleza kwamba, hivi karibuni kumekuwa na ongezeko la matumizi ya njia ya kikosi kazi katika miradi ya umma hasa katika ujenzi wa shule, vituo vya afya, majengo ya Serikali na ujenzi wa nyumba zinazomilikiwa na Serikali.

Alisema, ongezeko hilo limepelekea baadhi ya maeneo hoja nyingi kuibuliwa juu ya ukiukwaji wa maadili ya ununuzi na usimamizi wa mikataba na hivyo kupelekea matumizi makubwa ya fedha wakati wa utekelezaji wake.

Mhandisi Masunya alieleza utafiti huo ulilenga kuangalia thamani ya fedha na kuona endapo njia hiyo ni njia sahihi kwa matumizi ya kutekeleza miradi ya maendeleo ili kuiwezesha Mamlaka kutoa ushauri sahihi kwa Serikali na wadau wengine wa maendeleo juu ya matumizi ya kikosi kazi.

“Tuliamua kufanya utafiti ili tuone kama njia hiyo ya Force Account ni salama kutumiwa na Serikali kutokana na hoja nyingi zinazoibuliwa sio tu na viongozi bali hata wananchi” alisema.

Mhandisi Masunya alisema yapo maeneo ambayo yamefanikiwa katika utekelezaji wa miradi kwa kutumia njia hii licha ya baadhi ya maeneo mengine kushindwa kufanya vizuri.

Mhandisi Masunya alieleza kuwa PPRA ndiyo Mamlaka yenye wajibu wa kusimamia ununuzi wa Umma nchini, hivyo ina wajibu wa kuhakikisha thamani ya fedha na uwazi katika ununuzi unaonekana. Akieleza zaidi kuhusu njia hiyo alisema Sheria imeweka wazi kuwa yapo mazingira yanayo weza kulazimu taasisi kutumia njia hiyo. Mazingira hayo ni kama taasisi inayotaka kutekeleza mradi inaona kazi hiyo sio kubwa na maeneo ya mradi huo ni mbali kufikika.

Mhandisi Masunya alizikumbusha taasisi kuwa kigezo cha muhimu ni lazima zihakikisha kuwa wapo wataalamu ndani ya taasisi wanaoweza kusimamia na kuifanya kazi hiyo kwa ufanisi.

Utafiti huo ulijumuisha miradi iliyofanywa katika sekta ya afya, maji na elimu kwa kutumia fedha za UVIKO – 19. Utafiti huo uliangalia pia pia kaguzi maalum zilizofanywa na Mkaguzi Mkuu na Mdhibiti wa fedha za Serikali (CAG) katika miradi ya sekta ya Elimu kwa mwaka 2020 na Kaguzi maalum zilizofanywa na PPRA katika sekta ya afya mwaka 2020.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoTangulizi

Haya hapa majina 12 ya familia moja waliofariki kwenye ajali Tanga

Spread the love  MAJINA 12 kati ya 17 ya waliofariki dunia katika...

Habari Mchanganyiko

Rais Samia awalilia 17 waliofariki ajalini wakisafirisha maiti

Spread the love  RAIS Samia Suluhu Hassan, ametuma salamu za rambirambi kwa...

Habari Mchanganyiko

Wanawake wachimbaji wajenga zahanati kuokoa afya za wakazi 2000

Spread the love  ZAIDI wakazi 2,000 wa kijiji cha Nyamishiga Kata ya...

Habari Mchanganyiko

Baada ya Congo DR, Somalia mbioni kujiunga na EAC

Spread the love  TAIFA la Somalia liko mbioni kuwa mwanachama rasmi wa...

error: Content is protected !!