Tuesday , 21 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Polisi, wananchi wafanya usafi
Habari Mchanganyiko

Polisi, wananchi wafanya usafi

Spread the love

JESHI la Polisi Wilaya ya Same mkoani Kilimanjaro wameshirikiana na wananchi kufanya usafi, ikiwa ni sehemu ya kukabiliana na magonjwa ya mlipuko. Anaripoti Mwandishi Wetu, Same…(endelea).

Akizungumza Katika zoezi hilo Mkuu Polisi  Wilaya ya Same (OCD) SSP Phinias Majula alisema wao kama jeshi la polisi wameona ni vyema kushirikiana na jamii kwenye zoezi la kusafisha mazingira kuepuka milipuko ya magonjwa kama kipindupindu lakini pia kuona sehemu zinakuwa safi na salama.

Ametoa wito kwa Watanzania kutunza mazingira safi na salama na kupendelea kufanya usafi kwenye eneo linalowazunguka ili kuepukana na magonjwa ya mlipuko.

Majula aliwaomba wananchi kuendelea kushirikiana na jeshi la polisi kwa kutoa taaarifa za uhalifu na wahalifu katika wilaya hiyo kwani ni jukumu lao kuwalinda wananchi na mali zao.

Ofisa Mtendaji Mkuu Mamlaka ya Mji Mdogo Same amesema kwa niaba ya mkurugezi mkuu wilaya ya Same Anastazia Tutuba ametoa shukrani za dhati kwa jeshi la polisi kushirikiana na wananchi kwenye shughuli za kijamii.

Pia ameliomba Jeshi la Polisi kuendelea na utamaduni wa kushirikiana na wananchi lengo ni kujenga husiano mzuri baina ya jeshi na wananchi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Hukumu mahakama kuu yabatilishwa kesi State Oil, Equity Bank Tz

Spread the loveMAHAKAMA ya Rufani, jijini Dar es Salaam, imebatilisha hukumu iliyotolewa...

Habari Mchanganyiko

Geita, Mwanza waongoza kwa mbwa

Spread the loveNaibu waziri wa Mifugo na Uvuvi, Alexander Mnyeti amesema taarifa...

Habari Mchanganyiko

Waziri aipongeza NBS kwa mafanikio

Spread the love  Naibu Waziri wa Fedha, Hamad Chande amepongeza Ofisi ya...

Habari Mchanganyiko

Balozi Nchimbi aonya maofisa utumishi kuacha uonevu

Spread the love  KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Balozi Dk....

error: Content is protected !!