February 26, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Polisi wampiga risasi mtuhumiwa utekaji watoto Arusha

Samson Petro kijana aliyeuwawa na Polisi. Picha ndogo Kamanda wa Arusha, Charles Mkumb

Spread the love

MTUHUMIWA aliyekuwa ameshikiliwa na Jeshi la Polisi Mkoani Arusha kwa kuhusika na utekaji na mauaji ya watoto wawili Maureen na Ikram amefariki dunia kwa kupigwa risasi wakati akijaribu kutoroka mikononi mwa polisi, anaandika Irene David.

Kijana huyo anayejulikana kwa jina la Samson Petro, alikiri kuhusika na matukio mbalimbali ya utekaji wa watoto katika mikoa mbalimbali ikiwemo Arusha na Geita kwa lengo la kujipatia fedha.

Samson alipigwa risasi wakati akijaribu kutoroka kituo cha polisi na mwili wake upo katika hospitali ya mkoa wa Arusha Mount Meru.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo , amekiri kutokea tukio hilo na kwamba mtuhumiwa alipigwa risasi baada ya kujaribu kuwakimbia polisi alipokuwa amepelekwa kuwaonyesha mtu anayedaiwa kuwa walikuwa wanashirikiana katika utekaji huo wa watoto.

error: Content is protected !!