RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amesema atawaondoa Makamanda wa Jeshi la Polisi wa Mikoa (RPC), watakaoshindwa kudhibiti vitendo vya uhalifu, hasa ujambazi wa kutumia silaha. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Rais Samia ametoa kauli hiyo leo Jumanne tarehe 18 Mei 2021, akifungua Kiwanda cha Ushonaji cha Polisi, Kurasini mkoani Dar es Salaam.
Kiongozi huyo wa Tanzania amesema udhibiti wa uhalifu huo, utakuwa miongoni mwa vigezo vya kuteua au kutengua uteuzi wa Ma-RPC, atakaoufanya hivi karibuni.
“Jeshi la Polisi mjipange vizuri kukabiliana na hawa wanaotaka kuwajaribu na hii sio hapa Dar Es Salaam, bali nchi nzima.
https://www.youtube.com/watch?v=048gTByfeQ0
Na hapa niwe mkweli kwamba, miongoni mwa vigezo nitakavyotumia kuteua au kutengua makamanda wa mikoa ni udhibiti wa vitendo vya ujambazi ikiwemo kutumia silaha,” amesema Rais Samia.
Rais Samia amesema “hii nayo itakuwa moja kati ya vigezo, najua IGP (Simon Sirro) umeniletea majina kadhaa kwa ajili ya kamisheni mbili, ya fedha na lojistiki na ile kamisheni nyingine. Lakini hiki kitakuwa kimoja kati ya vigezo nitakavyotumia.”
Aidha, Rais Samia amemuagiza Inspekta Jenerali wa Polisi (IGP), Simon Sirro, aweke mikakati ya kudhibiti vitendo vya ujambazi.

“Changamoto za kiusalama bado zipo nielekeze wanaojaribu kina cha maji kwa kutaka kurejesha vitendo vya ujambazi hapa nchini, waache. Nampongeza IGP tarehe 8 Mei alikutana na Maafisa wa Polisi kuweka mikakati kukabiliana nao,” amesema Rais Samia na kuongeza:
“Ni matumaini yangu tutaona matunda ingawa bado tunasikia vijitaarifa taraifa hawa watu wanaendelea kubonyeza, naomba muwe wagumu wanapobonyeza pasibonyee, mliweza kule nyuma hamna sababu ya kushindwa sasa hivi.”
Leave a comment