Saturday , 25 March 2023
Home Gazeti Habari za Siasa Serikali yataja kinachokwamisha mradi Mchuchuma na Liganga
Habari za Siasa

Serikali yataja kinachokwamisha mradi Mchuchuma na Liganga

Mgodi wa Makaa ya mawe
Spread the love

 

SERIKALI ya Tanzania, imesema kinachokwamisha utekelezaji rasmi wa Mradi Unganishi wa Madini ya Chuma na Makaa ya Mawe ya Liganga na Mchuchuma, mkoani Njombe, ni majadiliano baina yake na mwekezaji. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dodoma … (endelea).

Hayo yamesemwa leo Jumanne tarehe 18 Mei 2021, bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Exaud Kigahe, akijibu swali la Mbunge Viti Maalum (CCM), Neema William Mgaya, aliyehoji lini Serikali itaanza utekelezaji wa mradi huo.

Kigahe amesema, Serikali iliamua kuunda Timu ya Majadiliano kati yake na muwekezaji Kampuni ya Sichuan Hongda (Group) Company Limited (SHGCL), baada ya kampuni hiyo kuomba vivutio ambavyo vinankinzana na baadhi ya Sheria za nchi.

“Ili kuendelea na utekelezaji wa mradi, mwekezaji aliomba vivutio (incentives), ambavyo vimeshindwa kutolewa na Serikali kwa sababu vinakinzana na baadhi ya Sheria za nchi,” amesema Kigahe.

Naibu Waziri huyo wa Viwanda na Biashara amesema ” kwa sasa, Serikali ipo katika hatua za uchambuzi wa mradi na kujiridhisha zaidi kuhusu namna bora ya kutekeleza mradi huu, ili kukidhi matakwa ya Sheria mpya Namba 5 na 6 za mwaka 2017 zinazolinda rasilimali za nchi.”

Kigahe amesema mradi huo utaanza kutekelezwa baada ya majadiliano hayo kukamilika.

“Kwa kuzingatia uchambuzi huo, Timu ya Serikali ya Majadiliano ilishaundwa na inaendelea kujadiliana na mwekezaji. Hivyo, utekelezaji wa mradi huu utaendelea mara baada ya kukamilika kwa majadilianobaina ya Serikali na Mwekezaji,” amesema Kigahe.

Amesema baada ya majadiliano hayo kukamilika mradi huo utatekelezwa kwa ubia kati ya Shirika la Maendeleo la Taifa (NDC) yenye hisa asilimia 20 na SHGCL (80%)

“Mradi huu unategemea kutekelezwa kwa ubia kati ya NDC na SHGCL , baada ya majadiliano kuhusiana na baadhi ya vipengele katika mkataba kukamilika,” amesema Kigahe.

Kigahe amesema “Katika utekelezaji wa mradi huu, utafiti wa kina ulikamilika 2012 na kubaini uwepo wa tani milioni 428 za makaa ya mawe katika eneo la Mchuchuma na tani milioni 126 za chuma katika eneo la Liganga.”

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za Siasa

Rais Samia aagiza iundwe kamati ya pamoja ya Mawaziri mradi wa BBT

Spread the love  RAIS Dk. Samia Suluhu Hassan, amewaagiza mawaziri kuunda kamati...

Habari za Siasa

Rais Samia apangua makatibu tawala mikoa, ateua Kamishna DCEA

Spread the loveALIYEKUWA Kamishna wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya, Gerald...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

M/kiti bodi ya wadhamini Chadema afariki dunia

Spread the loveMWENYEKITI wa Bodi ya Wadhamini ya Chama cha Demokrasia na...

Habari za Siasa

Zitto: Nikifa Ado atavaa viatu vyangu

Spread the love  KIONGOZI Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Zitto Kabwe...

error: Content is protected !!