May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simba yaingia kambini haraka, kuivutia kasi Kaizer Chiefs

Wachezaji wa Simba

Spread the love

 

KIKOSI cha Simba kimeingia kambili leo asubuhi kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa marudiano wa robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Kaizer Chiefs ya Afrika, utaochezwa Jumamosi ya tarehe 22 Mei, 2021. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea).

Timu ya Simba imerejea nchini ikitokea Afrika Kusini katika mchezo wa kwanza uliopigwa Jumamosi iliyopita ambapo walipoteza kwa mabao 4-0, na hivyo watatakiwa kushinda mabao 5 na kuendelea kwenye mchezo wa marudiano ili waweze kufuzu.

Baada ya kuwasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Mwalimu Nyerere, Afisa Habari wa klabu ya Simba, Haji Manara amesema wachezaji walipewa muda wa kupumzika kwa siku ya jana, hivyo leo wataingia kambini.

Haji Manara, Msemaji wa Simba

Kuelekea mchezo huo wa marudiano kocha wa klabu ya Simba, Didier Gomes alinukuliwa akisema kuwa wanahitaji kuwa bora ili waweze kupindua matokeo kwenye mchezo huo.

“Jambo lolote linawezekana kwenye mpira, hatujafurahia matokeo, lakini bado tuna matumaini, muhimu kuamini kwamba tunaweza kubadili matokeo, kama tunataka kupata matokeo kwenye mchezo wa marudiano lazima tuwe bora zaidi,” alisema Gomes.

Kwenye mchezo huo wa Jumamosi kuna uwezekano mkubwa wa kuchezwa bila mashabiki kufuatia Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) kutoa maelezo ya kuwa kuanzia hatua hii ya robo fainali na kuendelea hakuna timu itakayocheza na mashabiki.

error: Content is protected !!