Friday , 3 May 2024
Home Kitengo Biashara NMB yatoa gawio la bilioni 45.5, Rais Samia apongeza
Biashara

NMB yatoa gawio la bilioni 45.5, Rais Samia apongeza

Spread the love

BENKI ya NMB imetoa gawio la Sh.  45.5 bilioni ikiwa ni gawio kubwa zaidi kuwahi kutolewa na taasisi ya kifedha kwa Serikali. Serikali inamiliki asilimia 31.8 ya hisa katika benki hiyo, huku asilimia zingine zikiwa zinamilikiwa na wadau kutoka sekta binafsi. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Akipokea gawio hilo, Rais Samia Suluhu Hassan ameipongeza Benki hiyo kwa kufanikiwa kuwa kiongozi katika kutengeneza faida katika utekelezaji wa majukumu yake, huku akitoa wito kwa taasisi nyengine za umma kujiendesha kwa ufanisi na ushindani ili kuleta tija kwa Taifa.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan akipokea mfano wa Hundi ya Sh Bilioni 45.5 (Gawio la Serikali) kutoka kwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna kwenye maadhimisho ya miaka 25 ya Benki ya NMB.

Akizungumza jana tarehe 17 Juni 2023 Jijini Dar es Salaam katika kuadhimisho miaka ya 25 ya Mafanikio ya Benki hiyo ambayo yamekwenda pamoja na kukabidhi gawio hilo, Rais Samia amesema serikali inaendelea kufanya jitihadi katika kuhakikisha mashirika yote ya umma yanafanya kazi kwa ufanisi.

Amesema kuwa mashirika yasiyo na faida yanashindwa kujiendesha na kuitia hasara Serikali.

 

“Tutafanya tathmini kupitia Msajili wa Hazina ambapo Serikali itayachukulia hatua na kuyafuta mashirika ambayo hayafanyi vizuri” amesema Rais Samia.

Waziri wa Fedha na Mipango, Dk. Mwigulu Nchemba amesema  kiasi cha gawio ambalo limetolewa na Benki ya NMB ni kikubwa ambacho hakijawai kutolewa na taasisi za serikali.

Dk. Nchemba amesema kuwa mafanikio ya Benki ya NMB ni taarifa njema katika kuhakikisha uchumi wa Tanzania unakuwa imara kwa kuongeza chachu katika ukuaji wake.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan akibonyeza kitufe kuashiria kufunga maadhimisho ya miaka 25 ya Mafanikio ya Benki ya NMB katika hafla iliyofanyika Mlimani City Jijini Dar es Salaam tarehe 17 Juni, 2023.

Amesema serikali ya awamu ya sita imeendelea na mageuzi katika sekta mbalimbali ikiwemo fedha kutokana na mazingira wezeshe yaliokuwepo.

“Hili linathibitishwa na Benki ya NMB kupitia gawio la leo (jana), ambapo kuna ulipaji wa kodi, utoaji wa ajira kutokana na uwekezaji mkubwa ambao umefanywa” amesema Dk. Nchemba.

Amesema kuwa katika bajeti ya mwaka 2023/2024 serikali imeweka trilioni moja ambayo inakwenda kutumika kukuza sekta binafsi.

“Wizara ya fedha inaipongeza Benki ya NMB kwa mafanikio katika kipindi cha miaka 25 na wamekuwa wadau wakubwa katika kuwa wabunifu na kuendelea kuwa kinara katika kutoa huduma katika sekta ya fedha” amesema Dk. Nchemba.

Afisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB, Ruth Zaipuna amesema kuwa katika kuadhimisho miaka 25 ya Mafanikio wametenga Sh 2.5 bilioni kwa ajili ya kujenga Shule ya Mfano katika eneo na mkoa ambao atapendekeza na Rais Samia kwa ajili ya kuunga jitihada katika sekta ya elimu nchini.

Zaipuna amesema kuwa lengo ni kuhakikisha sekta ya elimu inapiga hatua na kupata mafanikio.

“Mafanikio ya Benki ya NMB yanapaswa kuendana jamii katika kuhakikisha wanatatua changamoto zilizopo.

“Benki ya NMB  itaendelea kuwa mdau mkubwa wa uwekezaji nchini kupitia kilimo na biashara,” amesema.

Amebainisha kuwa wamefanikiwa kutoa mikopo Sh 5.2 trilioni kwa ajili  ya wakulima, wafanyabiashara biashara wadogo  pamoja na watu binafsi.

“Mwaka huu tumefanya maboresha katika hospital ya Taifa ya Muhimbili katika hodi ya kujifungulia wakina mama kwa kununua vifaa mbalimbali pamoja na vitanda” amesema Zaipuna.

Naibu Cavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT), Sauda Msemo amesema kuwa wanaendelea kutekeleza majukumu yao ikiwemo dhamana ya kusimamia sera na utulivu wa uchumi nchini pamoja kuweka mazingira wezeshi kwa ajili ya kukuza uchumi.

Msemo amesema kuwa serikali kupitia BOT wanaendelea kuchukua hatua mbalimbali ili kuhakikisha huduma za kifedha zinawafikia wananchi kwa gharama nafuu.

Hata hivyo ameipongeza Benki ya NMB kwa jitihada kubwa ambazo wamefanya kwa kuboresho na kufanya mabadiliko na kufanikiwa kuwa na mtaji mkubwa na kutengeza faida.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Biashara

Cash Days Promo mamilioni yanakusubiri, cheza kupitia Meridianbet kasino 

Spread the love  JIANDAE kwa mshangao wa kustaajabisha Meridianbet kasino ya mtandaoni...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yazindua huduma maalum kwa wastaafu

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua huduma maalum kwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yazindua akaunti ya Kikundi

Spread the loveBenki ya NMB imezindua akaunti ya kikundi yenye  maboresho makubwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyakazi waidai STAMICO mishahara ya bilioni 1

Spread the loveWALIOKUWA wafanyakazi wa mgodi wa Shirika la Madini la Taifa...

error: Content is protected !!