UBONGO Kids waliotamba na katuni za watoto za Ubongo Kids na Akili na Me, sasa wamekuja na hadithi mpya za watoto wa Afrika iliyopewa jina la Nuzo na Namia. Anaripoti Mwandishi Wetu, Dar es Salaam … (endelea).
Kipindi hicho kipya kimezinduliwa leo tarehe 17 Juni, 2023 Century Cinema Mlimani City jijini Dar es Salaam ambapo baadhi ya wadau wamepata nafasi ya kukikona kipindi hicho kwa mara ya kwanza.
Hadithi hiyo ambayo itakuwa inahusu watoto wawili Nuzo na Namia ambao ni mapacha wenye umri wa miaka 7 wanaoishi na wazazi wao ambao walikuwa na ukaribu mkubwa na bibi yao aliyekuwa anawasimulia hadithi za safari zake katika nchi mbalimbali za Afrika.
Michael Baruti, Mkurugenzi wa Ubunifu wa Ubongo Kids, amesema kipindi hicho kitakuwa na Episode 13 ambazo zitakuwa inaonyeshwa katika televisheni ya EATV na Azam TV kuanzia tarehe 19 Juni, 2023.
Baruti amesema hadithi za Nuzo na Namia zitagusa utamaduni wa nchi mbalimbali za Afrika ambazo watoto hao wamefika kutokana na kusoma vitabu vya bibi yao aliyesafiri katika nchi hizo na wao wakafanya hivyo.
“Nuzo na Namia ni habithi ambazo ndani yake zinafundisha, hivyo nashauri watoto hata wakubwa wasiwaze kuikosa kwani itawajengea uwezo mkubwa kutokana na simulizi hizo,” amesema Baruti.
Naye Paul Masele, Mkurugenzi wa Uzalishaji wa Ubongo Kids amesema kupitia hadithi za Nuzo na Namia watapata fursa ya kujifunza kuwajengea uwezo wa kudadisi na kuhoji ikiwa pamoja na kutabiri kile kinachokuja mbele hali ambayo itawajenga hata watakapokuwa wakubwa.
Leave a comment