Friday , 26 April 2024
Home Habari Mchanganyiko NMB yakabidhi msaada vifaa tiba hospitali Pemba, Rais Mwinyi…
Habari Mchanganyiko

NMB yakabidhi msaada vifaa tiba hospitali Pemba, Rais Mwinyi…

Spread the love

BENKI ya NMB imetoa msaada wa vifaa tiba mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni tisa kwa Hospitali ya Wilaya ya Micheweni Pemba ikiwa ni utekelezaji wa azma yake ya kusaidia utoaji wa huduma bora za afya. Anaripoti Mwandishi Wetu… (endelea).

Mchango wa benki hiyo unaenda sambamba na maadhimisho ya miaka 59 ya Mapinduzi ya Zanzibar mwaka huu.

Rais wa Zanzibar na mwenyekikti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi (wapili kulia) akipokea moja ya viti venye magurudumu kutoka kwa Meneja wa Biashara wa Zanzibar wa Benki ya NMB, Naima Shaame (watatu kushoto) wakati akizindua hospitali ya wilaya ya Micheweni, Kaskazini Pemba. Benki ya NMB imetoa msaada wa vifaa venye thamani ya zaidi ya shilingi milioni tisa katika uzinduzi wa Hospitali hiyo.

Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na mashuka 200, vitenganisha wodi 10, viti venye magurudumu vitano kwaajili ya kusaidia wagonjwa na mashine tatu za kupimia presha.

Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi msaada huo iliyofanyika katika Hospitali ya Wilaya ya Micheweni Pemba jana, Meneja wa NMB Tawi la Zanzibar, Naima Said Shaame alisema mchango wa benki hiyo unatokana na dhamira yake ya kusaidia ujenzi wa Taifa lenye afya bora.

“Sisi kama Benki ya NMB, tunaamini kuwa watu wenye afya njema wana tija hivyo wanaweza kushiriki katika mchakato wa kujenga taifa lenye afya bora. Kwa maana hiyo Benki kwa miaka saba iliyopita imekuwa ikishughulikia baadhi ya vifaa muhimu vya matibabu na ukarabati wa miundombinu kutoka kwa hospitali mbalimbali nchi ili kuboresha afya za wagonjwa. Mchango wetu kwa Hospitali ya Wilaya ya Micheweni leo ni ushuhuda wa hili,” Shaame alisema.

Rais wa Zanzibar na mwenyekikti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi (wapili Kulia) akipokea maelekezo kutoka kwa Meneja wa Biashara wa Zanzibar wa Benki ya NMB, Naima Shaame (watatu kushoto) kabla ya kukabidhiwa msaada wa vifaa vya hospitali wakati akizindua hospitali ya wilaya ya Micheweni, Kaskazini Pemba. Benki ya NMB imetoa msaada wa vifaa venye thamani ya zaidi ya shilingi milioni tisa katika uzinduzi wa Hospitali hiyo.

Shaame alisema benki yake inatoa kipaumbele kwa sekta ya afya nakusistitza kuwa sekta hiyo ni moja ya nguzo kuu za Mpango wa Uwajibikaji kwa Jamii wa benki hiyo na kuongeza kuwa benki hiyo inawajibika kwa asilimia moja ya faida baada ya kodi (PAT) kugharamia mipango mbalimbali ya kijamii katika maeneo yake ya kipaumbele ikiwemo afya, elimu na dharura.

Alisema Benki ya NMB imechangia kwa kiasi kikubwa katika hospitali mbalimbali nchini na kuongeza kuwa michango ya benki hiyo inaleta mabadiliko makubwa katika kuinua viwango vya utoaji wa huduma za afya nchini kote.

“Kama mbia wa maendeleo, tutaendelea kufanya kazi na Serikali na washirika wengine katika kuleta maendeleo yenye maana katika jamii tunazofanyia kazi,” alisema Shaame

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk Hussein Mwinyi aliyepokea vitu hivyo kwa niaba ya Hospitali ya Wilaya aliishukuru benki hiyo kwa ukarimu wake na kuongeza kuwa uzinduzi wa Hospitali ya Wilaya ya Micheweni ni njia bora ya kuadhimisha miaka 59 ya Mapinduzi ya Zanzibar mwaka huu.

“Hii ni miongoni mwa hospitali kumi ambazo tumepanga kuzizindua mwaka huu katika Wilaya zote zikiwemo Unguja na Pemba. Hatua itakayofuata ni kujenga hospitali za mikoa na tunatarajia kuanza na Mjini Magharibi Unguja na tutaendelea na mikoa mingine. Tutajenga hospitali ya Taifa Zanzibar na mara tu itakapokamilika, hakutakuwa na haja ya kuwahamisha wagonjwa kutoka Zanzaibar hadi Tanzania Bara au nje ya nchi,” Dk Mwinyi alisema.

Aliwataka watoa huduma wa Hospitali hiyo ya Wilaya kutoa huduma bora na kuongeza kuwa huduma kwa wateja ni sehemu muhimu katika utoaji wa huduma za afya.

Waziri wa Afya Zanzibar Mhe, Nassor Ahmed Mazrui alisisitiza dhamira ya Wizara yake ya kutunza miundombinu katika Hospitali ya Wilaya ya Micheweni ili kutoa huduma bora za afya kwa Wazanzibari wote bila ya ubaguzi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

Habari Mchanganyiko

NBC yakabidhi vitanda Shule ya Polisi Moshi

Spread the loveBenki ya NBC imekabidhi msaada wa vitanda 28 kwa Shule...

error: Content is protected !!