Thursday , 2 May 2024
Home Habari Mchanganyiko NMB yaahidi neema ya meza, viti shule ya Sekondari ya Kumbukumbu ya Sokoine
Habari Mchanganyiko

NMB yaahidi neema ya meza, viti shule ya Sekondari ya Kumbukumbu ya Sokoine

Spread the love

 BENKI ya NMB ipo mbioni kutafuta ufumbuzi wa kudumu wa kumaliza changamoto ya upungufu wa meza na viti kwa walimu wa shule ya sekondari ya Kumbukumbu ya Sokoine iliyopo wilaya ya Mvomero  hali ambayo inalazimu walimu kutumia madawati ya wanafunzi katika shughuli zao za kila siku shuleni hapo. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Benki hiyo imeahidi kutoa msaada wa meza 30 na viti 30 vyenye thamani zaidi ya shilingi milioni 4 ndani na miezi mitatu ikiwa ni dhamira yake ya kumaliza tatizo hilo.

Akizungumza wakati wa mahafali ya kwanza ya kidato cha sita wilayani humo, Meneja wa Benki ya NMB kanda ya Kati, Nsolo Mlozi alisema benki imedhamiria kuchangia maendele endelevu ya kijamii nchin kote ikiwa ni utekelezaji wa mpango wa benki hiyo wa kurudisha kwa jamii inapofanyia kazi.

Nsolo alisema benki yake inatambua mchango wa serikali katika shule hiyo hivyo wao kama benki wanaunga juhudi hizo kwani wamekuwa na utaratibu wa kutenga fungu la kusaidia jamii katika sekta ya elimu, afya na majanga yanayoikumbuka kila mwaka kama sehemu ya kurejesha faida kwa jamii.

“Kila mwaka benki ya NMB imekuwa ikitenga sehemu ya faida yetu baada ya kulipa kodi serikalini na mwaka huu benki imetenga kiasi cha Sh6.6bilioni ambazo zinasaidia jamii katika sekta ya elimu, afya na majanga na shule hii ya Kumbukumbu ya hayati Edward Moringe Sokoine tutatoa msaada wa meza 30 na viti 30 ili kumaliza tatizo la ukosefu wa meza na viti inayowalazimu walimu kutumia madawati ya wanafunzi kugeuza meza na viti katika shughuli zao za kila siku,” alisema Nsolo.

Nsolo ambaye alikuwa mgeni rasmi katika mahafali hayo, amewataka wanafunzi hao kujiandaa zaidi katika mitihani ya taifa ya kuhitimu elimu ya kidato cha sita huku akiwataka watakaporudi majumbani baada ya kumaliza mitihani hiyo kuwa na tabia nzuri ili wale wataochaguliwa kwenda chuo na JKT kuendeleza nidhamu, bidii na juhudi ikiwa sehemu ya kuenzi mienendo ya hayati, Edward Sokoine aliyeishi katika misingi hiyo na mingine.

Awali, katika risala ya wahitimu kidato cha sita iliyosomwa na Boniface Lodovick (20) alisema shule hiyo inakabiliwa na changamoto ya uhaba wa mashine ya kuzalisha mitihani (Photocopy Machine na Printing Machine), uchache wa vitabu hasa kwa kidato cha tano na sita kama hesabu, uchumi, jiografia, kingereza na historia.

Kwa upande wa Mkuu wa shule hiyo, Gosbert Rwagasira alisema licha ya serikali kuwezesha mambo mengi mazuri zipo changamoto ambazo zinapaswa kutafutia ufumbuzi wa haraka kama kujengwa kwa daraja la kudumu ili wanafunzi na walimu kuondokana na adha ya kutotumia daraja la muda pindi mvua kubwa zinaponyesha daraja hilo hushindwa kutumika.

“Tunalo daraja la muda linalotenganisha kati ya mabweni, ofisi za kiutala na madarasa kwani nyakati za mvua kubwa daraja hilo halipitiki kwa sababu maji hupita juu na kwa usalama zaidi tunalazimika kuzunguka zaidi eneo hilo na kuchelewa kufika ofisini ama wanafunzi darasani kujengwa daraja la kudumu itakuwa mkombozi kwetu na ahadi ya NMB ya kutupatia meza 30 na viti 30 itaondoa changamoto pia ya walimu kutumia madawati ya wanafunzi kugeuza meza na viti,” alisema Rwegasira.

1 Comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yang’ara maonesho OSHA

Spread the loveBenki ya NMB imebeba tuzo ya kampuni bora kwenye sekta...

Habari MchanganyikoKimataifa

Ruto amteua Kahariri kuwa mkuu wa majeshi

Spread the loveRAIS wa Kenya, William Ruto, amemteua Jenerali Charles Muriu Kahariri,...

Habari Mchanganyiko

Chongolo aonya viongozi vijiji kutouza NIDA kwa wageni

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Songwe, Daniel Chongolo amewaonya viongozi wa...

Habari Mchanganyiko

TUCTA, OSHA wataka kampuni za madini kuiga ubunifu wa GGML

Spread the loveSHIRIKISHO la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA) pamoja na Wakala...

error: Content is protected !!