Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Neema yanukia Kilimanjaro, waitaliano waja kuchimba shaba
Habari Mchanganyiko

Neema yanukia Kilimanjaro, waitaliano waja kuchimba shaba

Spread the love

 

Shirika la Taifa la Madini (STAMICO) limesaini mkataba wa makubaliano ya awali na Kampuni ya Suness Limited ya Italia kwa ajili ya kuendeleza mradi mkubwa wa Shaba katika Mkoa Kilimanjaro. Anaripoti Mwandishi Wetu – Roma, Italia… (endelea)

Suness Limited ni kampuni ya Kiitaliano inayojishughulisha na uchimbaji madini na Kampuni hiyo imeonesha utayari wa kushirikiana na STAMICO katika kuendeleza kwa pamoja mradi wa shaba.

Akizungumza baada ya kusaini mkataba huo leo tarehe 4 Disemba jijini Roma Italia, Mkurugenzi Mtendaji wa STAMICO Dk. Venance Mwasse amesema mkataba umesainiwa kupitia jukwaa la biashara na uwekezaji lililofanyika Jijini Roma Italia tarehe 02 – 03 Disemba 2021.

Pamoja na mambo mengine, STAMICO wameweza kuelezea juu ya mradi wa mkubwa wa shaba unaopatikana katika Mkoa wa Kilimanjaro ambapo pia mwekezaji ameonesha nia ya kuingia ubia na STAMICO.

“Shirika lina mradi wake mkubwa wa Shaba mkoani Kilimanjaro wenye kiasi kikubwa cha mashapu ya Shaba na kupitia jukwa la wafanyabiashara na uwekezaji lililofanyika Roma – Italia, tumewaeleza juu ya mradi huo na wenzetu wameonesha kuvutiwa na mradi huo na tukakubaliana kusaini makubaliano ya awali na baadae watakuja Tanzania ili kwa pamoja twende kwenye eneo la mradi husika na mwishowe tuingie katika makubaliano ya pamoja ya kuendeleza mradi huo,” amesema Dk. Mwasse.

Naye Rais wa Kampuni ya Sunles, Sandro Calo amesema kuwa amefurahishwa na utiaji saini wa awali wa mkataba wa makubaliano kwa ajili ya kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kuendeleza kwa pamoja mradi wa Shaba.

“Nimefurahia kuanza kwa makubaliano haya mapya ambayo yataleja matokeo chanya kati ya nchi ya Tanzania na Italia na naahidi kuendeleza ushirikiano huu kwa maslahi mapana ya pande zote mbili katika sekta hii ya madini,” amesema Calo.

Utiaji saini wa makubaliano hayo umeshuhudiwa na Naibu Waziri, Wizara ya Madini Prof. Shukrani Manya, Balozi wa Tanzania Nchini Italia, Mahmoud Thabiti Kombo, Mkurugenzi Idara ya Diplomasia ya Uchumi katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Edwin Rutageruka pamoja na Mkurugenzi wa Kampuni ya Utalii ya Zanzibar Classic Safaris, Yussuf Salim Njama.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyakazi waidai STAMICO mishahara ya bilioni 1

Spread the loveWALIOKUWA wafanyakazi wa mgodi wa Shirika la Madini la Taifa...

AfyaHabari Mchanganyiko

200 wapimwa afya na GGML katika maonesho ya OSHA

Spread the loveZAIDI ya watu 200 jijini Arusha wamejitokeza kupimwa afya na...

Habari Mchanganyiko

Mfanyakazi CRDB atoa sababu za kubambikiwa kesi, hukumu Mei 30

Spread the love  MFANYAKAZI wa Benki ya CRDB, Ibrahim Masahi (40) ameieleza...

Habari Mchanganyiko

Waziri Ummy atangaza Tanzania kuwa kitovu cha utalii tiba

Spread the loveSERIKALI imesema imedhamiria kuifanya Tanzania kuwa kitovu cha matibabu ya...

error: Content is protected !!