May 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Rais Samia ateua DC, ahamisha 2

Spread the love

RAIS wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amemteua Dadi Horace Kolimba kuwa Mkuu wa Wilaya (DC) ya Karatu mkoani Arusha. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Uteuzi huo, umetangazwa leo Jumamosi, tarehe 4 Desemba 2021, na Jaffar Haniu, Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais Ikulu.

Kolimba anakwenda kuchukua nafasi ya Abbas Juma Kayanda ambaye amehamishiwa Wilaya ya Moshi, Mkoa wa Kilimanjaro.

Kayanda amekwenda kuchukua nafasi ya Said Mtanda ambaye Rais Samia amemhamishia Wilaya ya Arusha.

Mtanda amekwenda kujaza nafasi iliyokuwa wazi, kufuatilia aliyekuwa mkuu wa wilaya hiyo, Sophia Mjema, kuteuliwa na Rais Samia kuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.

error: Content is protected !!