May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Nabi kuikosa Simba

Nasriddine Nabi, Kocha wa Yanga (katikati)

Spread the love

 

KOCHA mkuu wa Yanga, Mohammed Nabi hatokuwa sehemu ya mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Simba kufuatia kuoneshwa kadi nyekundu kwenye mchezo wa Robo Fainali wa michuano ya kombe la Shirikisho la Azam dhidi ya Geita. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea). 

Nabi alioneshwa kadi hiyo mara baada ya kuingia katika sintofahamu na mwamuzi wa akiba mara baada ya dakika 90 za mchezo huo kukamilika na kujiandaa kwenda kwenye hatua ya mikwaju ya penati.

Mchezo huo ambayo Yanga ilibuka kidedea kwa ushindi wa penati 7-6, mara baada ya dakika 90 timu zote kufungana bao 1-1.

Nabi atalazimika kukaa nje la benchi ya Yanga katika michezo miwili ijayo, kwa mujibu wa kwnuni na adhabu zake zinaingia mpaka kwenye michezo ya Ligi Kuu.

Kwenye hatua ya nusu fainali, Yanga itacheza na mshindi kati ya Simba na Pamba ambao mchezo huo ulipangwa kuchezwa Jumatano tarehe 13 Aprili 2022, lakini umehailishwa na utapangiwa tarehe nyingine.

error: Content is protected !!