May 28, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Simba yaweka Ubingwa rehani, yalazimishwa sare na Polisi

Spread the love

 

KLABU ya Simba ni kama imeweka ubingwa wake wa Ligi Kuu Tanzania Bara rehani, baada ya kulizimishwa suluhu na kikosi cha Polisi Tanzania. Anaripoti Mwandishi Wetu, Kilimanjaro … (endelea).

Mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania Bara mzunguko wa Pili umepigwa majira ya saa 10 hii leo tarehe 10 Aprili 2022, kwenye uwanja wa Ushirika Moshi.

Sare hiyo imefanya kutengeneza wigo wa alama 10, kati ya Simba na vinara wa Ligi klabu ya Yanga huku kila mmoja akiwa amecheza michezo 19 mpaka sasa.

Simba kwa sasa imefikisha pointi 41, kwenye nafasi ya pili huku Yanga wakiwa na pointi 51 wakiongoza Ligi hiyo kwa miezi saba.

Katika mchezo huo, Kocha mkuu wa kikosi cha Simba, Pablo Franco Martin aliamua kupumzisha wachezaji wake watano wa kikosi cha kwanza kwa ajili ya mchezo ujao wa kombe la Shirikisho hatua ya robo fainali dhidi ya Orlando Pirates ya Afrika Kusini.

Mchezo huo utapigwa Jumapili ya tarehe 17 2022, majira ya saa 1 usiku kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam huku mchezo wa marudiano ukitarajiwa kupigwa Soweto Afrika Kusini tarehe 24 Aprili 2022.

Mara baada ya Simba kumalizana na Orlando itarejea kwenys muendelezo wa Michezo ya Ligi Kuu Tanzania Bara ambapo Tarehe 30 Aprili watashuka dimbani dhidi ya Yanga.

Mchezo huo ambao pengine unaweza kuamua hatma ya Yanga kutwa taji hilo ambalo wamelikosa kwa miaka minne, kama watapata ushindi na kutengeneza utofauti wa alama 13

error: Content is protected !!