Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Mzee Malecela aipa mbinu Serikali kukomesha ushoga
Habari Mchanganyiko

Mzee Malecela aipa mbinu Serikali kukomesha ushoga

Spread the love

MWANASIASA nguli nchini ambaye pia Waziri Mkuu mstaafu,John Samwel Mallecela ameitaka serikali kuweka sheria ngumu au kifungo cha muda mrefu kwa mtu yeyote atakayejihusisha na vitendo vya mapenzi ya jinsia moja ikiwemo ushoga. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma… (endelea).

Malecella ametoa kauli hiyo leo tarehe 9 Aprili 2023 muda mfupi baada ya kumalizika kwa ibada ya kumbukizi ya kufufuka kwa Yesu Kristo iliyofanyika katika Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Central Tanganyika jijini Dodoma.

Waziri mkuu mstaafu John Malecela (kulia) akisalimiana na mmoja wa wachungaji baada ya kumalizika kwa ibada ya Pasaka iliyofanyika Kanisa Kuu la Angalikan Roho Mtakatifu Dayosisi ya Central Tanganyika leo jijini Dodoma.

Mwanasiasa huyo mkongwe amesema anasikitishwa na vitendo hivyo ambavyo wapo baadhi ya wanavishabikia ili kuipotosha jamii kujihusisha na masuala ya ushoga.

“Nalaani kabisa vitendo vya ushoga na usagaji, ni dhambi ambayo inakatazwa katika vitabu vya dini na ni dhambi ambyo haiwezi kusameheka.

“Nitamshangaa sana Mkristo anayeshabikia ushoga wakati jambo limelaaniwa, ni jambo la giza… ni sawa na uchawi na ujambazi hivyo kuna kila sababu ya serikali kuweka sheria kali au kifungo cha mrefu kwa mtu yoyote ambaye atajihusisha na ushoga” amesema Malecela.

Aidha, Askofu wa kanisa la Anglikana Dayosisi ya Central Tanganyika, Dk.Dikson Chilongani amewataka viongozi wa juu serikalini kuhakikisha wanapambana na vitendo vya rushwa ambavyo vinaonekana kushamiri zaidi nchini.

Amesema kuwa nchi haiwezi kuwa na maendeleo ya kiuchumi kama haitapambana na kuzuia vitendo vya rushwa ambavyo vinadhoofisha upatikanaji wa haki.

“Rushwa inaonekana kushamiri kila mahali …mahakamani na sehemu za utoaji wa huduma jambo ambalo linasababisha wanyonge kukosa haki zao za msingi na kuwanufaisha matajiri ambao wanatumia fedha zao  kupora mali za watu” ameeleza Dk. Chilongani.

Katika hatua nyingine amewataka viongozi wa dini kutotumia mahubiri ya upotoshaji kwa watu kwa kuwaaminisha kwenye suala la miujiza badala ya kufanya kazi.

Amesema kuwa wahubiri wameanzisha injili za kuwaaminisha watu kuwa watapokea miujiza bila kuwaambia ukweli kuwa hakuna muujiza ambao unaweza kutokea kama mtu hajafanya kazi.

“Maandiko matakatifu yanafundisha wazi kuwa kila mtu afanye kazi na asiyefanya kazi asile leo hii mtu anakuambia utapokea muujiza bila kufanya kazi hayo ni maubiri ya upotoshaji.

“Israel ni nchi pekee yenye ukame mkubwa lakini kwa  sasa ni nchi pekee yenye teknolojia kubwa zaidi na hiyo inatokana na watu wake kufanya kazi kwa bidii na kuwa wabunifu zaidi.

“Nchi haiwezi kuwa na maendeleo kama itakuwa na watu wavivu wazembe ambao wanategemea miujiza bila kufanya kazi ambayo itachangia kuongeza pato la taifa au mtu binafsi.

“Tatizo la uchumi wa nchi si la Rais wa nchi au Serikali yake, tatizo ni uvivu na uzembe wa wananchi wenyewe kwa kutopenda kufanya kazi ambazo zitawaingizia kipato cha uhakika”ameeleza.

Sambamba na hayo amewataka watanzania kwa ujumla wao kuhakikisha wanapambana na suala la ushoga na asiwepo mtu wa kuliunga mkono jambo hilo kwani ni chukizo mbele za Mungu.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

RPC Dodoma akabidhiwa bunduki mbili za wahalifu

Spread the love  Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa ya Kulevya...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yazindua huduma maalum kwa wastaafu

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua huduma maalum kwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yazindua akaunti ya Kikundi

Spread the loveBenki ya NMB imezindua akaunti ya kikundi yenye  maboresho makubwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyakazi waidai STAMICO mishahara ya bilioni 1

Spread the loveWALIOKUWA wafanyakazi wa mgodi wa Shirika la Madini la Taifa...

error: Content is protected !!