July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mwili wa Dk. Mengi watua Kilimanjaro

Spread the love

MWILI wa Dk. Reginald Mengi, aliyekuwa mwenyekiti wa kampuni zilizo chini ya IPP Group, tayari umewasili kwenye Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA). Anaripoti Hamisi Mguta, Kilimanjaro … (endelea).

Viongozi mbalimbali wa serikali, mila, ndugu, jamaa na marafiki mkoani humo, wamejitokeza kuulaki mwili wa Dk. Mengi ambaye ulibebwa na Shirika la Ndege la Precision asubuhi ya leo tarehe 8 Mei 2019 na kutua KIA.

Dk. Mengi anatarajiwa kuzikwa kesho tarehe 9 Mei 2019 kijijini kwake Machame, Moshi baada ya shughuli ya ibada na taratibu zingine kufanyika.

Mfanyabiashara huyo (Dk. Mengi), alifariki dunia usiku wa kuamkia tarehe 2 Mei 2019 Dubai, Falme za Kiarabu.

error: Content is protected !!