July 5, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mbunge Msigwa amshitaki RC Hapi kwa waziri

Mkuu wa Mkoa wa Mara, Ally Hapi

Spread the love

MBUNGE wa Iringa Mjini, Peter Msigwa (Chadema) amemshitaki Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Ally Hapi kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu. Anaripoti Danson Kaijage, Dodoma … (endelea).

Mch. Msigwa amesema kuwa, Hapi amekuwa akisababisha wataalamu wa afya kukimbia hivyo kukosesha wananchi wa Iringa huduma bora za afya.

Amefikisha mashitaka hayo bungeni alipokuwa akichangia hotuba ya wizara hiyo juu ya Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka wa Fedha 2019/20.

Amesema kuwa, ziara inayofanywa na Hapi imekuwa ni ya kuwadhalilisha wataalamu, jambo ambalo limesababisha wataalamu wengi wa afya kukimbia.

Mbali na watumishi wa idara ya afya kukimbia na kusababisha adha kubwa kwa wale wanaohitaji huduma, Msigwa ameitaka serikali ieleze kama watumishi wa umma ni sahihi kuingiliwa na watendaji wa kisiasa.

Msigwa amesema kuwa, inasikitisha kuona viongozi wa kisiasa kugeuka kuwa mwiba kwa watumishi wa umma, kwa kutumia majukwaa kuwadhalilisha.

error: Content is protected !!