Saturday , 3 June 2023
Home Habari Mchanganyiko Mwanamke afariki akifanya mapenzi kichakani
Habari Mchanganyiko

Mwanamke afariki akifanya mapenzi kichakani

Spread the love

 

Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 37 anakabiliwa na mashtaka ya mauaji baada ya mpenzi wake aliyefahamika kwa jina moja la Milca (48) kufariki dunia wakati wakifanya mapenzi kichakani eneo la Mbita katika Kaunti ya Homa Bay nchini Kenya. Inaripoti Mitandao ya Kimataifa … (endelea).

Kwa mujibu wa mtandao wa TUKO, tukio hilo limetokea Jumapili jioni tarehe 19 Machi 19 2023 baada ya wapenzi hao waliokuwa wanarejea nyumbani kuamua kuingia kwenye kichaka eneo la Got Rateng kwa ajili ya kufanya kitendo hicho walipokuwa wametoka kunywa pombe.

Chifu wa eneo hilo Bernard Ouma amesema kuwa wawili hao awali walikuwa wameonywa wasishiriki tendo wakiwa wamelewa lakini hawakutii.

Amesema mshtakiwa anashikiliwa na Jeshi la Polisi nchini humo baada ya kukiri chanzo cha kifo hicho.

Hata hivyo, inadaiwa kuwa mwanaume huyo amemrithi Milca baada ya kifo cha mume wake kama ilivyo utamadumi wa wakazi wa eneo hilo, ambapo mwanamke anaruhusiwa kurithiwa pale mumewe anapofariki.

“Baada ya kifo cha Milca alijaribu kuuzika mwili wake na ndipo tukamkamata mshtakiwa.

“Kuna wakati niliwaita na kuwaonya kuhusu kufanya mapenzi sehemu zisizo na staha hasa baada ya kunywa pombe, waliendelea na ninafikiri hilo linaweza kuwa chanzo cha maafa haya,” amesema Chifu Ouma.

Mwili wa marehemu umepelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Homa Bay huku uchunguzi zaidi ukiendelea.

7 Comments

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Magunia 731 ya bangi yakamatwa, mamia ya hekari yateketezwa Arumeru

Spread the love  MAMIA ya magunia ya madawa ya kulevya aina ya...

Habari MchanganyikoTangulizi

Bosi NIC apandishwa kizimbani, akabiliwa na mashitaka 365

Spread the love  ALIYEKUWA Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Bima la Taifa...

Habari Mchanganyiko

Serikali yakabidhi eneo la mahakama ya Afrika ya haki za binadamu

Spread the loveSerikali kupitia Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa...

Habari Mchanganyiko

Udhamini wa NMB mikutano ya ALAT wafikia 1.2 bilioni

Spread the loveBENKI ya NMB imeendelea kufanya kazi kwa karibu na Asasi...

error: Content is protected !!