Tuesday , 19 March 2024
Home Habari Mchanganyiko NMB yamwaga mamilioni kuimarisha afya, elimu katika Kanda ya Kati
Habari Mchanganyiko

NMB yamwaga mamilioni kuimarisha afya, elimu katika Kanda ya Kati

Spread the love

BENKI ya NMB imetoa msaada vifaa mbalimbali kwa sekta za elimu na afya vyenye thamani ya shilingi milioni 39 kwa Wilaya za Kanda ya Kati zikiwemo Mpwapwa, Kondoa na Chemba ikiwa ni utekelezaji wa sehemu ya dhamira yake ya kurudisha kwa jamii. Anaripoti Mwandishi Wetu…(endelea).

Walionufaika katika Wilaya ya Mpwapwa ni pamoja na Shule za Msingi Iyoma na Mpwapwa zilizopokea madawati 100 kwa jumla yenye thamani ya shilingi milioni 10.

Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Dk. Sophia Kizigo(Kushoto) akipokea moja ya madawati kutoka kwa Meneja wa Benki ya NMB kanda ya Kati, Nsolo Mlozi (kulia) wakati ya makabidhiano ya madawati 100 kwa shule mbili za msingi wilayani hapo. Benki ya NMB imefanya makabidhiano ya vifaa mbalimbali vya Afya na Elimu venye thamani ya zaidi ya milioni 39 kwa shule na vituo vya afya mkoani Dodoma. Wapili kulia ni meneja wa NMB tawi la mpwapwa, Nathaniel Mwamfupe, wapili kushoto ni kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Mpwapwa, Noel Kaka na katikati ni mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa, George Fuime.

Walionufaika katika Wilaya ya Kondoa kwa upande mwingine ni pamoja na Hospitali ya Wilaya ya Kondoa ambayo iliyopokea mashuka 200 yenye thamani ya shilingi milioni 6m, Shule za Sekondari Bicha, Masange, Kimaha na Dalai zilizopokea meza na viti 50 kila moja vyenye thamani ya shilingi milioni 5 huku Shule ya Msingi Lembo ikipata vifaa vya kuezekea vyenye thamani ya shilingi milioni 5.6.

Kwa upande wa sekta ya afya, benki hiyo pia ilitoa msaada wa vifaa mbalimbali vyenye thamani ya shilingi milioni 12.3 katika Hospitali ya Wilaya ya Chemba ambavyo ni pamoja na mashuka 64, vitanda vya kujifungulia vinne, vitanda vya kawaida vya wagonjwa 10, na magodoro kumi miongoni mwa vifaa hivyo kwa lengo la kuasaidia kuimarisha utoaji huduma hospitalini hapo.

Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi msaada huo, Meneja wa Kanda ya Kati wa Benki ya NMB, Nsolo Mlonzi alisema msaada huo unathibitisha dhamira ya benki hiyo ya kurudisha kwa jamii inapofanyia kazi na kuongeza kuwa benki hiyo imetenga shilingi bilioni 6.2 kusaidia uwekezaji  katika uwekezaji katika miradi mbalimbali ya ya kijamii hususan katika sekta zake za kipaumbele ikijumuisha elimu, afya na dharura mwaka huu.

“Katika Benki ya NMB, elimu na afya ni vipaumbele vyetu muhimu kwani tunaamini elimu ni ufunguo wa maisha bora ya baadaye ya watoto, lakini bila vifaa vya kutosha, watoto wengi hupata shida kujifunza. Kama wadau wakubwa wa maendeleo, leo tunakabidhi madawati na meza ili kuimarisha mazingira ya kujifunzia kwa wanafunzi wetu,” Mlonzi alisema.

Wakati wa hafla hiyo Mlonzi aliwataka wanufaika wa michango ya benki hiyo kuvitumia vyema vitu vilivyotolewa kwa ajili ya vizazi vijavyo.

Naye Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa, Sophia Kizigo wakati akipokea msaada huo kwa niaba ya wilaya yake aliipongeza benki hiyo kwa ukarimu wake na kuongeza kuwa, “msaada huo umekuja wakati mwafaka kwetu huku tukijitahidi kuboresha mazingira ya kujifunzia mashuleni,”

Kizigo alibainisha kuwa madawati 100 yaliyotolewa na benki katika wilaya yake yatasaidia kwa kiasi kikubwa yatasaidia wanafunzi kujifunza katika mazingira mazuri zaidi na kuyataka wafanyabiashara Na na kampuni nyingine zinazoofanya biashara wilayani humo kuunga mkono juhudi zake za maendeleo.

“Tumefurahi sana kwa mchango huu na ni Imani yetu kuwa sasa wanafunzi wetu hawatabanana tena kama ilivyokuwa. Sasa watastarehe wanapojifunza,” alisema.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Diwani, wananchi wengine 463 wahama Ngorongoro

Spread the loveMakamu mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Ngorongoro ambaye pia...

ElimuHabari Mchanganyiko

GGML yawapa mbinu wanafunzi Geita Boys kufikia malengo ya kitaaluma

Spread the loveKampuni ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imetoa mafunzo maalumu...

Habari MchanganyikoKimataifa

Shule zafungwa kutokana na ongezeko la joto

Spread the loveSUDAN Kusini imeamuru kufungwa kwa shule zote kuanzia leo Jumatatu,...

Habari Mchanganyiko

Bunge laja na Marathon kuchangia ujenzi wa sekondari

Spread the loveBUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania linatarajia kukusanya fedha...

error: Content is protected !!