Friday , 9 June 2023
Home Habari Mchanganyiko Taasisi ya kuendeleza uchimbaji mdogo imetakiwa kushirikiana na serikali
Habari Mchanganyiko

Taasisi ya kuendeleza uchimbaji mdogo imetakiwa kushirikiana na serikali

Kamishna wa Madini Dk. AbdulRahman Mwanga
Spread the love

 

KAMISHNA wa Madini Dk. AbdulRahman Mwanga ameitaka Taasisi ya Kuendeleza Uchimbaji Mdogo (FADev) kushirikiana na Serikali katika utekelezaji wa majukumu yake ili Serikali na jamii itambue kazi zinazotekelezwa na taasisi hiyo. Anaripoti Mwandishi Wetu …(endelea).

Rai hiyo, imetolewa leo tarehe 22 Machi 2023 alipokutana na Uongozi wa taasisi ya FADev ambao umefika kwa lengo la kujitambulisha na kueleza majukumu yanayofanywa na taasisi hiyo kuendeleza uchimbaji mdogo katika kikao kilichofanyika ofisi za wizara Mtumba jijini Dodoma.

Dk. Mwanga ameitaka FADev ishirikiane na Serikali ili kujenga mahusiano mazuri katika utekelezaji wa majukumu mbalimbali na kusaidia kuepusha kuingiliana na majukumu hayo mara kwa mara.

Aidha, ameitaka FADev kuendelea kuilinda taasisi hiyo kwa kuheshimu taratibu na misingi iliyowekwa na nchi ambayo inalinda utu wa watanzania katika majukumu yao.

Kwa upande wake, Katibu Mtendaji wa FADev Mhandisi Theonestina Mwasha amesema kuwa, inaendelea kutekeleza miradi inayokuza na kuimarisha uzalishaji wa dhahabu katika mikoa ya Geita na Shinyanga.

“Tunafanya mafunzo katika maeneo ya uchimbaji, tunatoa elimu shirikishi kwa jamii inayozunguka migodi nakuanzisha mchakato wa kutoa elimu ya kuongeza thamani kwa ushirikiano wa wadau,” amesema Mhandisi Mwasha.

Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Kuendeleza Uchimbaji Mdogo (FADev) Mhandisi Theonestina Mwasha

Akizungumzia kuwaendeleza wachimbaji wadogo Mhandisi Mwasha amesema, taasisi imetoa vifaa vya uchimbaji migodi kwa vikundi mbalimbali walivyofanya navyo kazi sambamba na kuimarisha vikundi vya wanawake 15 katika mikoa ya Geita na Shinyanga.

Amesema, hadi sasa taasisi ya FADev imefanikiwa kutoa mbinu za ujasiriamali kwenye maeneo ya uchimbaji madini, mafunzo ya utunzaji wa mahesabu, mafunzo ya ukusanyaji na utunzaji wa taarifa na matumizi sahihi ya kemikali zinazotumika kwenye uchenjuaji.

Pia imefanikiwa kutoa mikopo isiyozidi milioni 15 kwa kila kikundi kwa vikundi vitatu kwa kushirikiana na benki ya NBC.

Kikao hicho, kimehudhuriwa na wataalam mbalimbali kutoka Wizara ya Madini, Tume ya Madini na Taasisi ya Jiolojia na Utafiti wa Madini Tanzania (GST).

1 Comment

  • KWA AJILI YA MASHINDANO YA MTU WA KWANZA KUWAHI PATIKANA DUNIANI – UKIONA VIPI TUMA KWENYE ANUANI HII

    H.E Ambassador
    Dr. Emmanuel John Nchimbi
    The Embassy of the United Republic of Tanzania
    10 ANAS Ibn Malek Street,
    Mohandessin,
    Cairo, Egypt
    Postal Code: 12411

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

Askari Polisi zaidi ya 100 wapigwa msasa wa udereva kukabiliana na ajali

Spread the love  KATIKA kuhakikisha wimbi la ajali za barabarani zinapungua kama...

Habari MchanganyikoTangulizi

Serikali yakana kuhamisha kwa nguvu jamii ya Kimasai Loliondo

Spread the loveWAZIRI wa Katiba na Sheria nchini Tanzania, Dk. Damas Ndumbaro,...

Habari Mchanganyiko

Tunduma watenga 60 milioni kujenga machinjio ya kisasa

Spread the loveHALMASHAURI ya mji Tunduma Imetenga kiasi cha Tshs Miloni 60...

Habari Mchanganyiko

Bilioni 17 kujenga bandari kavu Tunduma

Spread the loveHALMASHAURI ya mji Tunduma iliyopo wilayani  Momba mkoani Songwe imepatiwa...

error: Content is protected !!