Friday , 3 May 2024
Home Habari Mchanganyiko Mwanafunzi wa Kenya ajiteka nyara na kudai kikombozi
Habari Mchanganyiko

Mwanafunzi wa Kenya ajiteka nyara na kudai kikombozi

Spread the love

POLISI katika mji mkuu wa Kenya, Nairobi, wamemkamata mwanafunzi wa udaktari anayedaiwa kughushi utekaji nyara wake mwenyewe ili kudai kikombozi kutoka kwa wazazi wake.

Kwa mujibu wa BBC Edwin Kamau (23), anatuhumiwa “kutoweka” siku ya Jumapili na kumpigia simu mamake siku chache baadaye kuomba fidia ya Ksh 70,000 (Tsh 1,380,000).

Awamu ya kwanza ya fidia hiyo ililipwa siku ya Jumatano, lakini polisi wanasema mwanafunzi huyo alienda kulewa nje kidogo ya jiji na mwanamke ambaye aliongeza kinywaji chake na kuiba pesa hizo.

Siku ya Alhamisi, alidai na kulipwa awamu ya pili ya fidia hiyo lakini akamatwa muda mfupi baadaye na pesa hizo zikapatikana zikiwa zimewekwa kwenye viatu vyake.

Polisi wanasema mwanafunzi huyo alikiri kufuja pesa zilizokuwa zikilipwa karo ya muhula uliopita na kughushi utekaji nyara wake ili kutafuta pesa. Mshukiwa anasubiri kufikishwa mahakamani.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

BiasharaHabari Mchanganyiko

NBC yazindua huduma maalum kwa wastaafu

Spread the loveBenki ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua huduma maalum kwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

NMB yazindua akaunti ya Kikundi

Spread the loveBenki ya NMB imezindua akaunti ya kikundi yenye  maboresho makubwa...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wafanyakazi waidai STAMICO mishahara ya bilioni 1

Spread the loveWALIOKUWA wafanyakazi wa mgodi wa Shirika la Madini la Taifa...

AfyaHabari Mchanganyiko

200 wapimwa afya na GGML katika maonesho ya OSHA

Spread the loveZAIDI ya watu 200 jijini Arusha wamejitokeza kupimwa afya na...

error: Content is protected !!