Saturday , 27 April 2024
Home Habari Mchanganyiko Mwabukusi ataja sababu 3 kukata rufaa kupinga hukumu kesi DP World
Habari MchanganyikoTangulizi

Mwabukusi ataja sababu 3 kukata rufaa kupinga hukumu kesi DP World

Wakili Boniface Mwabukusi
Spread the love

 

WAKILI Boniface Mwabukusi anayeongoza jopo la mawakili waliosimamia kesi ya kikatiba iliyofunguliwa na wananchi wanne mkoani Mbeya, ametangaza kukata rufaa kupinga hukumu iliyotolewa leo Alhamisi Mahakama Kuu, Kanda ya Mbeya Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya kwa kutupa mbali kesi hiyo waliyoifungua tarehe 3 Julai mwaka huu. Anaripoti Mwandishi Wetu, Mbeya … (endelea).

Mwabukusi na wenzake walifungua kesi hiyo kupinga vifungu vya mkataba wa ushirikiano wa kiuchumi kati ya Serikali ya Tanzania na Dubai ikiwamo kwenye uwekezaji bandari za Tanzania kupitia kampuni ya DP World.

Hata hivyo, katika hukumu iliyosomwa leo tarehe 10 Agosti 2023 na jopo la Majaji wa Mahakama Kuu, Masjala Kuu, mahakama hiyo imedai mkataba huo haukukiuka vifungu vya Katiba wala sheria za nchi.

Kesi hiyo namba 05/2023 iliwahusisha Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Dk. Eliezer Feleshi; Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Prof. Makame Mbarawa; Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi na Katibu wa Bunge, Nenelwa Mwihambi.

Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kusomwa kwa hukumu hiyo, Wakili Mwabukusi amefafanua kuwa mambo matatu ambayo wanaamini yanawalazimu kwenda mahakama ya rufaa kwa mujibu wa wateja wake.

Amesema suala la kwanza ilikuwa kupata tafsiri sahihi ya hicho walichokiita makubaliano lakini mahakama baada ya kupata nafasi imetupa mbali hivyo wameshauriana na wateja kwamba hawakubaliani nao kwa misingi ya kisheria.

“Kwanza moja mahakama haitakiwi ku- refrain au kutoa order pale inapogundua kuna tatizo. Inapogundua kuna tatizo inatakiwa kutoa amri,” amesema.

Amedai baadhi ya maeneo ya mkataba huo mahakama imesema haiwezi kutoa amri kwa sababu kuna vifungu vya marekebishio jambo ambalo sio sahihi kwani mahakama ikigundua kosa inatakiwa kulitolea amri.

“Mkataba huu umekiuka sheria za maliasili kwa kuelekeza migogoro yote ikiwamo ile ya ndani inatakayotokana na mikataba midogo ya nje, na ile inayohusiana na ile mikataba isikiliziwe nje ya Tanzania kwa sheria za Tanzania lakini na mamlaka zilizo nje ya Tanzania,” amesema na kuongeza kuwa;

“Ukishagundua hilo tatizo unachotakiwa nikutoa amri kuhusiana na hilo sio ku-withhold kwa sababu hiyo nayo tunakwenda ku-challenge katika mahakama ya rufaa kwa kuzingatia maelekezo ya wateja wetu,” amesema.

Akizungumzia jambo la pili, Mwabukusi amesema mahakama inasema inakubaliana nao kwamba Dubai haina sifa kwa mujibu wa mkataba wa kimataifa inaofahamika kama Montevideo convetion.

“Mahakama imesema kwamba sisi hatujatoa instrument… si sahihi na tulishatoa maelezo tulishaonesha ni kwanini Dubai haina instruments(sifa kuwa nchi), kwa sababu instrumenst iliyotolewa ipo kwenye sehemu ya makubaliano… kwa hiyo ilitakiwa itolewe mamlaka au order kulingana na zile instruments zilizopo kule,” amesema.

Amesema sifa za zilizopo kwenye mkataba huo kuitambua Dubai kuwa nchi ni za Umoja wa Falme za Kiarabu

“Utakuta ni ya mtu tu ameandika, kwa hiyo tunaamini mahamama ingetakiwa itoe tu amri kwamba kwa sababu hana uwezo na ana utata wa uwezo tayari huo sio mkataba,” amesema.

Jambo la tatu ambalo linawasukuma kwenda Mahakama ya Rufaa, amesema ni suala la maliasili ya nchi ambayo Tanzania iliridhia kupitia azimio la umoja wa mataifa na kuweka vigezo vya namna ya kusimamia rasilimali zake.

Amedai sheria ipo bayana kwamba mambo yote yanayohusu maliasili ya Tanzania yatashughulikiwa ndani ya Tanzania.
“Kwa hiyo hata ukiusoma mkataba wa Vienna unaeleza bayana kwamba sehemu ambazo nchi imeweka sheria za kimsingi ambazo ni kama permanent sovereignty basi sheria za nchi zile zitaheshimiwa kwa mkataba huo wa kimataifa,” amedai.

Ameongeza kuwa wanashauriana na wateja wao na kuchambua hukumu hiyo kitaalaam waone namna ya kwenda mahakama ya rufani.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari za SiasaTangulizi

Prof. Lipumba ajitosa kuviunganisha vyama vya siasa Burundi

Spread the love  MWENYEKITI wa Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD), Prof. Ibrahim...

Habari Mchanganyiko

Wakili: Ukimpa zawadi mwenza marufuku kumpora hata mkiachana

Spread the love  WANANDOA na watu waliko kwenye mahusiano ya kimapenzi, wamekumbushwa...

Habari Mchanganyiko

Majaliwa: Mvua zimesababisha vifo vya watu 155, kuendelea hadi Mei

Spread the love  WAZIRI Mkuu, Kassim Majaliwa amesema mvua kubwa za El-Nino...

Habari Mchanganyiko

Exim Bank yatoa  vitanda kwa shule ya Jeshi la Polisi Moshi

Spread the love  BENKI ya Exim imekabidhii  seti ya vitanda kwa Shule...

error: Content is protected !!