November 27, 2022

Uhuru hauna Mipaka

Mtoto (3) afikishwa kortin Jerusalem

Spread the love

MOHAMMED Rabi ‘Aliani (3), amefikishwa katika Kituo cha Polisi cha Yerusalem kuhojiwa akituhumiwa kuwapiga mawe wanajeshi wa Israel. Inaripoti mitandao ya kimataifa…(endelea).

Ni baada ya kikosi cha Jeshi la Israel kuvamia makazi yao yaliyopo katika Mji wa Al-Sawiya, Jerusalem ya Mashariki.

Uongozi wa Israeli Jumatatu ya tarehe 29 Julai 2019, ulitoa agizo la kumtaka Rabi afikishwe katika kituo cha polisi cha Yerusalemu ili kuhojiwa na polisi.

Wapalestina wakazi wa Mji wa al-‘Isawiya, walifuatana na mtoto Rabi kwenda kwenye kituo hicho cha polisi huku wakifanya maandamano.

Jumuiya ya Palestina ya kutetea haki za wafungwa, imeomba uchunguzi ufanyike juu ya tukio hilo.

Mkuu wa jumuiya hiyo, Meja Jenerali Kadri Abu Bakr amelaani uongozi wa Israeli kwa kumtaka mtoto huyo wa miaka 3 kuhojiwa kwenye kituo cha polisi, akisisitiza kwamba kitendo hicho ni uhalifu dhidi ya watoto wa Palestina.

Abu Bakr amehoji ukimya wa jumuiya ya kimataifa juu ya ukiukaji wa sheria za kimataifa juu ya Haki za Watoto unaofanywa na Israel. Na kwamba, umesababisha muendelezo wa unyanyasaji na uonevu wa watoto hao.

error: Content is protected !!