Tuesday , 18 June 2024
Home Habari Mchanganyiko Polisi: Mhandisi Lwajabe amejinyonga
Habari Mchanganyiko

Polisi: Mhandisi Lwajabe amejinyonga

Kamanda Lazaro Mambosasa, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam
Spread the love

JESHI la Polisi, Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limeeleza, Mhandisi Leopord Lwajabe, aliyekuwa Mkurugenzi Msaidizi wa Miradi ya Umoja wa Ulaya (EU) katika Wizara ya Fedha alifariki kwa kujinyonga. Anaripoti Mwandishi Wetu … (endelea).

Kauli hiyo imetolewa na Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa wakati akizungumza na  wanahabari leo tarehe 31 Julai 2019.

Kamanda Mambosasa amesema, uchunguzi wa awali uliofanyika katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili, umebainisha kwamba chanzo cha kifo cha Lwajabe ni kujinyonga.

“Mwili wa marehemu ulihamishiwa Muhimbili kwa uchunguzi zaidi na ilibainika kifo cha marehemu kilisababishwa na kujinyonga. Chanzo cha kujinyonga kwake bado kinachunguzwa,” amesema Kamanda Mambosasa.

Aidha, Kamanda Mambosasa amesema, marehemu Lwajabe aliacha Notebook ofisini kwake aliyoandika ujumbe wa mgawanyo wa mali zake kwa familia yake.

“Tarehe 29.07.2019 wafanyakazi waligundua kuwa marehemu aliacha Notebook juu ya meza ofisini kwake ambapo ilikuwa na ujumbe wa mgawanyo wa mali zake kwa familia yake na kwamba, kwenye msiba wake ng’ombe wane wachinjwe,” amesema Kamanda Mambosasa.

Kamanda Mambosasa ameeleza, mfanyakazi mwenzake na Lwajabe aliwaeleza polisi ya kwamba muenendo wa marehemu ulibadilika kwa kupunguza kasi ya utendaji kazi.

“Hata hivyo, taarifa toka kwa mfanyakazi mwenzake alisema, marehemu alikuwa amepunguza kasi katika utendaji jambo ambalo sio kawaida yake na hata kazi zingine za muhimu alikuwa akimpa kaimu wake kuzifanya,” amesema Kamanda Mambosasa.

Akieleze mazingira ya kupatikana kwa mwili wa Lwajabe, Kamanda Mambosasa  amesema, Jeshi la Polisi lilifika eneo la tukio baada ya kupewa tarifa za tukio hilo na Mwenyekiti wa Kijiji cha Mgoza, Mohamed Said (68).

Kamanda Mambosasa amesema, baada ya polisi kufanya uchunguzi eneo la tukio, walibaini kwamba eneo hilo halikuwa na viashiria vyovyote vya kujitetea wakati wa tukio, pia mwili haukuwa na jeraha lolote isipokuwa shingoni kulikuwa na kamba ya nailoni aliyotumia kujinyonga.

Amesema, polisi waliufanyia upekuzi mwili wa Mhandisi Lwajabe na kukuta fedha kiasi cha Sh. 90,000 kwenye mfuko wa suriali upande wa kulia na Sh. 98,000 upande wa kushoto, pochi yenye Dola za Marekani 10 katika mfuko wa nyuma, kitambulisho cha mpiga kura na saa ya mkononi.

“Wananchi waliitwa ili kuutambua mwili ambapo hakuna aliyeweza kuutambua. Baada ya hapo mwili ulichukuliwa na kuhifadhiwa Hospitali ya Wilaya ya Mkuranga kwa utambuzi na uchunguzi wa daktari na kufunguliwa jalada kosa la kujinyonga, na upelelezi uliendelea ikiwa ni pamoja na kuwatafuta wanandugu wa marehemu,” amesema Kamanda Mambosasa.

Kamanda Mambosasa amesema, mnamo tarehe 29 Julai 2019 ndugu wa marehemu Lwajabe walikuja kuutambua mwili wake.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari Mchanganyiko

CoRI: Waandishi wa habari 16,000 hawana mikataba ya ajira Tz

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chamalila amemthibishia...

Habari MchanganyikoHabari za SiasaTangulizi

RC Chalamila: Nimeacha ubabe

Spread the loveMKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chamalila amemthibishia...

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Rais Samia atoa ujumbe mzito Sikukuu Eid Al Adha

Spread the loveKATIKA kusherehekea Sikukuu ya Eid Al Adha, Rais wa Tanzania,...

BiasharaHabari Mchanganyiko

Wachimba chokaa 300 waomba mikopo kuondokana na matumizi ya kuni

Spread the loveKUNDI la vijana wanaojishughulisha na uchimbaji wa chokaa katika kijiji...

error: Content is protected !!