April 12, 2021

Uhuru hauna Mipaka

Mtanzania aomba Ziwa Victoria libadilishwe jina

Spread the love

DAKTARI Abdullah Hasnuu Makame, leo tarehe 6 Desemba 2019, amefikisha azimio la kubadilisha jina la Ziwa Victoria, katika Bunge la Afrika Mashariki (EALA). Anaripoti Regina Mkonde … (endelea).

Katika azimio lake hilo, Dk. Makame amelitaka Baraza la Mawaziri la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), kubadili jina la ziwa hilo, ili lipewe jina la Ki-Afrika.

Akikazia hoja yake hiyo, Dk. Makame amesema kubadilishwa kwa jina la Ziwa Victoria, itakuwa hatua muhimu katika kuzitambulisha nchi za Afrika, kwamba ziko huru kutoka kwa utawala wa kikoloni.

“Haya ni matukio ya uhuru, mabadiliko ya jina ni hatua inayoibua mahitaji ya kujitambulisha sisi kama wa Afrika, walio huru kutoka utawala wa kikoloni,” ameandika Dk. Makame katika ukurasa wake wa Twitter, leo tarehe 6 Desemba 2019.

Ziwa Victoria ni ziwa kubwa katika ukanda wa Afrika Mashariki, ambapo linapaka na nchi ya Tanzania, Kenya na Uganda.

error: Content is protected !!