Thursday , 13 June 2024
Home Habari Mchanganyiko Msaidizi wa Membe anashikiliwa polisi tuhuma za utakatishaji fedha
Habari Mchanganyiko

Msaidizi wa Membe anashikiliwa polisi tuhuma za utakatishaji fedha

SACP Lazaro Mambosasa, Kamanda wa Kanda Maalum Dar es Salaam
Spread the love

JEROME Luanda, Msaidizi wa Bernard Membe, Mgombea Urais wa Tanzania kupitia Chama cha ACT-Wazalendo anashikiliwa Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam tuhuma za utakatishaji fedha. Anaripoti Regina Mkonde, Dar es Salaam … (endelea).

Hayo yamesemwa leo Alhamisi tarehe 17 Septemba 2020 na Lazaro Mambosasa, Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam alipokuwa akizungumzia kushikiliwa na Luanda.

Membe kupitia ukurasa wake wa Twitter, alidai Luanda alitekwa muda mchache baada ya kutua naye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere Dar es Salaam, wakitokea Dubai, walikokwenda wiki iliyopita.

Membe aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya ndani kati ya mwaka 2005 hadi 2015 katika utawala uliopita wa Rais mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete aliandika “Tukio la kutekwa kwa msaidizi wangu Jerome Luanda jana (juzi) mara baada ya kutua kwenye kiwanja cha Kimataifa cha JK Nyerere international Airport nitalizungumzia kwa undani saa 10 kamili leo (jana). Nimewapa wahusika wanaodhani siwajui masaa matatu wamwachie akiwa mzima na salama.”

Hata hivyo, Kamanda Mambosasa amesema mtuhumiwa huyo anahojiwa kwa kosa la utakatishaji fedha.

Benard Membe, Mgombea Urais kwa tiketi ya ACT-Wazalendo

“Mtuhumiwa huyo amekamatwa, amekamtwa uwanja wa ndege anahojiwa kwa kosa la kutakatisha fedha,” amesema Kamanda Mambosasa.

Kuhusu madai ya mtuhumiwa huyo kutekwa na wasiojulikana, Kamanda Mambosasa amesema ni ya uongo kwa kuwa Jeshi la Polisi lilimkamata msaidizi huyo wa Membe akiwa uwanjani hapo.

“Mtuhumiwa huyo nasema hivyo kwa sababu kuna watu wameanza kusambaza mara amekamatwa na watu wasiofahamika, mara nimezunguka vituo vyote vya polisi sijamuona sasa mi namshangaa anayesema hivyo sababu huwezi kuzunguka vituo bila kuingia ‘rock up’ kujua kama mtuhumiwa yupo au hayupo, tunayefahamu ni sisi,” amesema Kamanda Mambosasa.

1 Comment

  • Kwani sheria si iko wazi kuwa polisi ni lazime wamfikishe mahakamani katika saa 24 au wamuachie?
    Membe nenda mahakamani ukadai itoe amri ya kuachiwa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Habari MchanganyikoHabari za Siasa

Wafungwa, mahabusu ruksa kupiga kura

Spread the loveTUME Huru ya Taifa ya Uchaguzi (INEC) imesema kuwa wafungwa,...

BiasharaHabari MchanganyikoHabari za Siasa

Deni la Serikali lafikia trilioni 91

Spread the loveWaziri wa Mipango na Uwekezaji Profesa Kitila Mkumbo amesema hadi...

BiasharaHabari Mchanganyiko

GGML yaahidi kuendelea kushirikiana na UDSM kudhamini tafiti, ubunifu

Spread the loveKAMPUNI ya Geita Gold Mining Limited (GGML) imeahidi kuendelea kushirikiana...

BiasharaHabari MchanganyikoHabari za Siasa

Marekani yasaka fursa uwekezaji sekta ya nishati Tanzania

Spread the loveNaibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Doto Biteko amekutana...

error: Content is protected !!