Saturday , 25 March 2023
Home Kitengo Michezo Ligi Kuu kuendelea kuwasha moto kesho
Michezo

Ligi Kuu kuendelea kuwasha moto kesho

Spread the love

MICHEZO ya Ligi Kuu Tanzania Bara kuendelea wikiendi hii kwa kuchezwa jumla ya mechi tisa, zitakazo chezwa katika viwanja tofauti tofauti, huku mabingwa watetezi klabu ya Simba wanatarajia kuwa katika Uwanja wa Mkapa jijini Dar es Salaam kuikabili Biashara United. Anaripoti Kelvin Mwaipungu, Dar es Salaam … (endelea). 

Simba ambayo ilitoka sare kwenye mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar itapata muda wa kujiuliza mbele ya Biashara Unite ambayo ilipata ushindi klwenye michezo yake miwili ya kwanza.

Mchezo mwengine wa kuvutia utaikutanisha klabu ya Yanga ambayo ipo ugenini kuikabili Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba siku ya jumamosi 19 septemba, 2020 mara baada ya kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mbeya City.

Yanga kwa sasa ipo nafasi ya sita kwenye msimao wa ligi huku watani zao Simba wakiwa kwenye nafasi ya nne, wote wakiwa na pointi nne hivyo mchezo huo utakuwa wa muhimu kwa upande wao katika kujitengenezea mazingira mazuri ya kuwa nafasi ya juu kwenye msimamo.

Kwa upande wa Kagera Sugar itakuwa na nafasi ya kujiuliza mbele ya Yanga mara baada ya kutoka saruhu ya bila kufungana dhidi ya Gwambina na kupoteza katika mchezo wa kwanza wa Ligi na hivyo kufanya timu hiyo kuwa na pointi moja na kushika nafasi ya 14 kwenye msimamo wa ligi.

Vinara wa Ligi hiyo klabu ya Kmc baaada ya kushinda katika michezo yake miwili waliocheza wakiwa kwenye Uwanja wa Nyumbani dhidi ya Tanzania Prisons na Mbeya City sasa watakuwa ugenini kwa mara ya kwanza kwenye mchezo dhidi ya Mwadui Fc kutoka Shinyanga ambao wametoka kupoteza kwenye mchezo uliopita dhidi ya Biashara United kwa bao 1-0.

Mchezo huo unatarajia kuchezwa siku ya jumatatu 21 septemba 2020, kwenye Uwanja wa Mwadui Complex Shinyanga.

Azam FC nao watakuwa ugenini kwa mara ya kwanza baada ya kushinda katika michezo miwili dhidi Polisi Tanzania na Costal Union na kuvuna pointi sita na kushika nafasi ya pili kwenye msimao, watasafiri kuelekea mkoani Mbeya na kucheza kwenye Uwanja wa Sokoine siku ya jumapili 20 Septemba, 2020 dhidi ya Mbeya City.

Ikumbukwe Mbeya City imepoteza michezo yake miwili ya kwanza kwa kukubali kichapo cha mabao 4-0 kutoka kwa KMC na bao 1-0 dhidi ya Yanga Afrika michezo yote ikipigwa Jijini Dar es Salaam na kuifanya timu hiyo kuburuza mkia.

Michezo ya awali itakayochezwa siku ya kesho Ijumaa 18 Septemba, 2020, itaikutanisha klabu ya Polisi Tanzania dhidi ya JKT Tanzania kwenye Uwanja wa Ushirika, huku Ihefu FC itamenyana na Mtibwa Sugar kwenye Uwanja wa Sokoine.

Siku ya Jumamosi Tanzania Prisons itakuwa nyumbani kwenye Uwanja wa Nelson Mandela, Rukwa kukipiga na Namungo FC ambao walipoteza kwenye mchezo uliopita kwa bao 1-0 dhidi ya Polisi kwenye Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa.

Siku ya Jumapili 20 septemba 2020 Coastal Union itavaana na Dodoma Jiji kwenye uwanja wa mkwakwani, Tanga.

Licha ya kuwa msimu wao wa kwanza kwenye Ligi Dodoma jiji imefanikiwa kuibuka na ushindi kwenye michezo yao miwili ya kwanza huku Coastal Union ikifungwa kwenye michezo yao miwili ya kwanza.

Mchezo wa mwisho kwa mzunguko wa tatu utapigwa siku ya Jumatatu 21 Septemba, 2020 kwenye Uwanja wa Mabatini, Pwani ambao utawakutanisha wenyeji wa mchezo huo Ruvu Shooting FC itakapo vaana na Gwambina.

Ligi Kuu Tanzania bara kwa msimu wa 2020/21 inashirikisha jumla ya timu 18, huku michezo hiyo itakuwa ikichezwa kuanzia siku ya Ijumaa mpaka jumatatu ili kutoa fursa kwa Azam TV kuonesha idadi ya michezo mingi.

Leave a comment

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Related Articles

Michezo

Yanga: Fedha za Rais Samia zinaleta ari kubwa

Spread the loveUONGOZI wa klabu ya Yanga, umesema fedha zinazotolewa na Rais...

Michezo

Simba Sc. yamvulia kofia Rais Samia, yamuahidi makubwa dhidi ya Horoya

Spread the loveWAKATI timu ya Simba ikiibuka na ushindi wa bao 3-0...

Michezo

Taasisi ya TKO na TFF yawapiga msasa makocha wa kike 54

Spread the love WAKATI Soka la wasichana likichipua kwa kasi Taasisi ya...

Michezo

Kimwanga CUP yazidi kutimua vumbi

Spread the loveMASHINDANO ya mpira wa miguu ya Kimwanga CUP ya kuwania...

error: Content is protected !!